Serikali
imetakiwa kuheshimu haki ya kikatiba ya kuwapa wananchi habari na
taarifa muhimu zinazowahusu bila ya kujali gharama za taarifa hizo kwa
kuwa ni jukumu lake kufanya hivyo.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na kituo cha sheria na haki za
binadamu kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi wake Bi. Imelda Urio na kuongeza
kuwa kusitishwa baadhi ya matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge
kwa kisingizio cha gharama ni kitendo cha makusudi kwa kuwanyima
wananchi taarifa muhimu toka kwa wawakilishi wao ambao ni wabunge.
Bi
Imelda Urio ameongeza kuwa muhimili wa bunge na viongozi wake lazima
wafanye kazi kiueledi na kuzuia mianya ya kuingiliwa na mihimili mingine
hususani serikali.
Aidha LHRC imelaani vikali kitengo cha kuzalilishwa kwa wabunge kwa kutolewa bungeni na mbwa wa jeshi la polisi,
Kwa
upande wa kaimu mkurugenzi wa utetezi na maboresho Bi. Anna Henga yeye
amesema kuwa haki yoyote haina gharama na ni jukumu la serikali kulipia
gharama hizo za matangazo ya bunge.
No comments:
Post a Comment