Baraza
la Waganga Tanzania (BAWATA) wameunga mkono tamko la Serikali la
kukataza waganga wa tiba asili kujitangaza katika vyombo vya habari.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Baraza la Waganga
Tanzania Shaka Mohamed Shaka alipokuwa akiongea na waandishi wa habari
kuhusu waganga wanaokiuka taratibu na sheria zilizowekwa na Serikali juu
ya utoaji huduma ya tiba asili nchini.
‘’Sisi
kama Baraza la Waganga Tanzania tukishirikiana na Serikali tunatoa wito
kwa vyombo vya habari wasitoe matangazo ya waganga wa tiba asili kwakua
jambo hili ni kosa kwa mujibu wa sheria”alisema Shaka.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Baraza hilo David Witekye ameiomba radhi
Serikali kutokana na tamko la Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Tiba
Asili Tanzania (SHIVYATIATA) Abdulraham Lutenga kwa kuitisha mkutano na
waandishi wa habari bila kushirikiana na kamati yake tendaji wala vyama
vinavyounda shirikisho hilo na kuwatetea wafanyabiashara wa tiba asili
ambao wamejivika kilemba cha utabibu asili.
“Kwa
niaba ya BAWATA, tunaiomba radhi Serikali kutokana na tamko la
Mwenyekiti wa SHIVYATIATA kupinga tamko la Serikali, tunaamini lile ni
tamko lake binafsi na sio la shirikisho”. alisema Wiketye.
Ameongeza
kuwa,wameafiki tamko la Serikali kuhusu upimaji na usajili wa dawa
asili na kupendekeza zoezi hili kuangaliwa upya ili kuwezesha watabibu
asilia kumudu gharama hizo.
Tamko
hilo lilitolewa baada ya kujitokeza kwa changamoto mbalimbali ikiwa ni
pamoja na watoa huduma wa tiba za asili kutozingatia Sheria, Kanuni na
miongozo mbalimbali inayohusu afya ya jamii.
No comments:
Post a Comment