Kuna utaratibu mpya ambao unakuja kuhusu
wasanii wa muziki kulipwa baada ya nyimbo zao kuchezwa kwenye vituo vya
TV na radio, wakati huohuo kuna neno mirabaha ambalo huenda umekutana
nalo na hujajua maana yake na linahusiana na nini.
Hii ndio maana ya mirabaha iliyoelezwa na Doreen Anthony Sinare ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) >> ‘Ni
kipato ambacho unakipata kutokana na kazi ambayo umeitengeneza…
inawezekana umeuza nakala, unatafsiri kazi, umekodisha au kutangaza..
pesa unayoipata ndio mrabaha‘- Doreen Sinare.
Hapa imetajwa idadi ya wasanii wa muziki waliosajiliwa COSOTA mpaka sasa>>> ‘Kwa kukadiria ni kama 21% waliosajiliwa, mtaani kuna nyimbo nyingi lakini hawajisajili‘- Doreen Sinare.
Vipi kuhusu ishu ya vituo vya TV na Radio kulipia nyimbo za wasanii, haitashusha muziki wa TZ? >> ‘Kisheria
inatakiwa muziki wa ndani upewe 60% hewani.. naamini muziki wetu ni
mzuri, nadhani haitokuwa hivyo tunavyofikiria… siamini kama kituo
kinaweza kumaliza siku bila kupiga wimbo wa ndani‘
No comments:
Post a Comment