Baada ya Canavaro kuvuliwa unahodha na kupewa Mbwana Samatta, haya ndio maamuzi yake magumu - LEKULE

Breaking

15 Jan 2016

Baada ya Canavaro kuvuliwa unahodha na kupewa Mbwana Samatta, haya ndio maamuzi yake magumu



Baada ya kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa January 10 kuamua kutangaza kumvua unahodha Nadir Haroub Canavaro na kutangaza kumpatia nafasi hiyo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayeichezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta, hali imekuwa tofauti kwa upande wa Canavaro.
Canavaro ambaye ameichezea timu ya taifa ya Tanzania kwa takribani miaka 10, ameamua kutangaza kustaafu kucheza timu ya taifa, Canavaro ametaja sababu kadhaa zilizomfanya afikie maamuzi hayo, ikiwemo sababu ya kuvuliwa unahodha bila ya heshima yoyote, licha ya kuitumikia timu hiyo kwa muda mrefu.
cannavaro sauz
“Sing’ang’anii na wala silazimishi kuwa nahodha, kikubwa ninachotaka ni kupewa heshima yangu kwa kuipeperusha vyema bendera ya timu ya taifa, “Kiukweli nimepokonywa unahodha bila ya heshima, ninajisikia vibaya kupokonywa unahodha kwa kupitia vyombo vya habari kitu ambacho siyo sahihi, hali hiyo imeshusha heshima yangu kwa kiwango kikubwa” >>> Canavaro

Hata hivyo Canavaro ametaja sababu nyingine iliyomfanya kuamua maamuzi ya kujitoa Taifa Stars, kwani baada ya mechi ya ugenini iliyochezwa dhidi ya Algeria na Taifa Stars kufungwa goli 7-0, lawama na maneno maneno yalimuangukia yeye kuwa ameisha na umri umemtupa mkono hivyo ameona awaachie vijana waendele kuichezea Taifa Stars.

No comments: