WAHITIMU 67 wasio katika Mfumo Rasmi watunukiwa vyeti katika kuwarasimisha katika ujuzi waliopata katika maeneo yao ya kazi.
Akizungumza
katika mahafali hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mafunzo na
Ufundi Stadi (VETA),Geofrey Sabuni amesema kuwa wataendelea kutoa
mafunzo hayo ili kuwatambua mafundi wa mitaani ambao wamekuwa
hatambuliki kutokana na kukosa mafanzo katika taasisi zinazotambulika.
Amesema
kuwa nia ya kuwafikia watu 5000 katika kurasimisha kazi wanazozifanya
kutokana na mchango mkubwa wa taifa huku wakiwa hawatambuliki.
Sabuni
amesema kuwa VETA itahakikisha inaendelea kutoa mafunzo kwa vijana
katika ujuzi mbalimbali pamoja na wale ambao hawako katika mfumo rasmi
kuwatambua.
Aidha
amesema kuwa katika jitihada zote kuna changamoto hivyo kwa wahitimu
lazima waendelee kuongeza ujunzi wa mafunzo ya muda mrefu katika kuwa
wabobezi huku wakiwa na vyeti vinavyoonyesha ujuzi.
Kaimu
Mkuu wa Chuo cha Veta Dar es Salaam,Violet Fumbo amesema katika mafunzo
wanayotoa wanatambulika sehemu zote kutokana na mafunzo hayo kuingizwa
katika mitaala.
Violet amesema katika mambo wanayoyafanya ni kutaka vijana kujituma katika ujuzi waliofanya kazi hiyo
Afisa
mitihani wa chuo cha ufundi cha VETA kilichopo Temeke,Elishawake Lema
akifungua sherehe za Mhafari kwa wanafunzi waliojiunga kozi ya muda
mfupi ambayo Veta wameshirikiana na na shilika la kazi Duniani (ILO) kwa
kutoa mafunzo hayo. mafunzo hayo ni Upishi, ufundi uwashi, ufundi wa
magari na upambaji.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha ufundi stadi cha Veta, Geofrey Sabuni
akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya muda mfupi katika chuo hicho leo
jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu
wa Chuo cha ufundi stadi cha Veta, Violet Fumbo kulia akisoma lisala
mbele ya wahhitimu na mgeni rasmi katika mahafari ya muda mfupi ya chuo
cha ufundi cha Veta leo jijini Dar es Salaam. waliokaa kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya mafunzo ya ufundi stadi (VETA), Geofrey Sabuni Mwakilishi wa Shirika la Kazi (ILO), Albert Okal na Afisa mitihani wa chuo cha ufundi cha VETA kilichopo Temeke,Elishawake Lema.
Mwakilishi
wa Shirika la Kazi (ILO), Albert Okal akizungumza na wahitimu wa chuo
cha mafunzo stadi ya ufundi cha Veta jinsi walivyo shirikiana na chuo
hicho ili kuondoa okosefu wa ajira kwa baadhi ya vijana walioweza
kufanikiwa kujiunga na kozi ya muda mfupi katika chuo hicho.
Walimu waliofanikisha mafunzo kwa wanafunzi na wahitimu wa leo katika chuo hicho.
Wahitimu wakisimsikiliza mgeni rasm katika mahafari hayo leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wanafunzi wakiongalia matisheti yao yakiwa na nembo ya shirika la
kazi duniani (ILO) leo katika mahafari ya mafunzo hayo.
Katika
mahafali hayo wametunukiwa vyeti vya kufuzu masomo yao katika chuo cha
mafunzo ya ufundi Stadi (VETA) leo jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa chuo wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wahitimu leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment