Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),
imeanza kukagua taasisi za umma kuhusu utekelezaji wa sheria inayozitaka
kuwatambua waajiriwa walionufaika na mikopo ya elimu ya juu.
Hadi
Mei mwaka jana, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
ilikuwa imekusanya Sh65.2 bilioni kati ya Sh123.8 bilioni zilizopaswa
kuwa zimerejeshwa.
Bodi hiyo iliwakopesha wanafunzi Sh1.8 trilioni
tangu mwaka wa masomo 1994/95 hadi Juni 2014 kati ya fedha hizo, Sh51
bilioni zilitolewa na iliyokuwa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na
Teknolojia.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, George Nyatega alisema
ili kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mikopo iliyoiva, CAG ameanza
kutekeleza matakwa ya kisheria ya ukaguzi kwenye taasisi za umma ili
kuwabaini wanafunzi waliopaswa kuanza kurejesha mikopo yao.
“Ni
imani ya HESLB kuwa waajiri katika utumishi wa umma watatoa ushirikiano
kwa ofisi ya CAG ili kuondokana na matatizo ya kisheria,” alisema.
Nyatenga
alisema sheria iliyoanzisha HESLB inazitaka taasisi zote za umma
kuijulisha kwa maandishi kuhusu waajiriwa wapya ndani ya siku 28 na bodi
kuthibitisha kama waajiriwa hao ni wanufaika wa mikopo au la.
Mkurugenzi
huyo alisema baada ya bodi kupokea taarifa na kuthibitisha kuwa
waajiriwa ni wanufaika wa mikopo, mwajiri atapaswa kuijulisha HELSB na
kuanza kukata sehemu ya mshahara wa mwajiriwa ndani ya siku 30.
No comments:
Post a Comment