BUNGE
limetoa idhini kwa mawaziri walioteuliwa na Rais John Magufuli ambao
hawajala kiapo cha ubunge kushiriki shughuli za kibunge.
Limesema
wateule wa Rais Magufuli katika nafasi za uwaziri ambao kwanza
waliteuliwa kuwa wabunge watakula kiapo cha ubunge wakati wa mkutano wa
pili wa Bunge la 11, ili kutimiza matakwa ya kikatiba na kanuni za Bunge
kabla ya kuanza rasmi kutekeleza majukumu yao ndani ya Bunge.
Msimamo
huo wa Bunge umetolewa jana na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah
kuhusu uhalali wa mawaziri hao kushiriki shughuli za kibunge kabla ya
kuapishwa.
Dk.
Kashilillah alisema Katiba na Kanuni za Bunge hazimzuii Rais kuteua
wabunge na kuwapa nafasi za uwaziri, wakati ambao Bunge halikutani na
badala yake amepewa mamlaka ya kikatiba katika Ibara ya 55 ya kuteua mtu
kuwa waziri na Ibara ya 56 inampa mamlaka ya kumwapisha.
Alisema kwa muktadha huo, Katiba na Kanuni za Bunge haziweki mipaka ya wakati wabunge kuchaguliwa au kuteuliwa.
“Rais
hafungwi na masharti yaliyo kwenye ibara ya 68 ya Katiba kuhusu
kuwaapisha wabunge kabla ya kuanza kushiriki shughuli za Bunge kwa
sababu tafasili ya shughuli za Bunge imewekwa wazi na Ibara ya 63 ambayo
kimsingi inasema ni shughuli za Bunge ndani ya Bunge na kamati zake.
“Hivi
sasa Kamati za Bunge bado hazijaundwa na Spika mpaka mkutano wa pili wa
Bunge la 11 utakapoanza Januari 26, mwaka huu. Lakini hata kama
itatokea kamati inafanya kazi zake kabla ya Bunge kukutana, kama kuna
waziri ambaye hajaapishwa kuwa mbunge, rais ana mamlaka ya kumkaimisha
waziri mwingine ambaye amekwishaapishwa kuwa mbunge kushikiri shughuli
hizo.
“Leo
nimeongea na waandishi wa habari wengi sana walionipigia simu
wakiulizia hili kwa sababu naona limekuwa na mjadala mkubwa. Haya mambo
ya kibunge ni vizuri kuyaelewa kwanza kwa sababu hata Kanuni za Bunge
zimetoa nguvu kwa kamati kujipangia utaratibu wake wa kazi na kuwaruhusu
watu ambao si wabunge au wabunge ambao si wa wajumbe wa kamati husika
kushiriki katika vikao,” alisema Dk. Kashilillah.
Alisema
kwa ruhusa hiyo iliyotolewa na Kanuni ya 117 (8), mawaziri walioteuliwa
na Rais Magufuli wanaweza kushiriki kwenye shughuli za Kamati za Bunge
pasipo kuhesabiwa kuwa ni wajumbe rasmi.
No comments:
Post a Comment