Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ametembelea Kituo cha
Kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji cha Mtera kwa lengo la kujionea hali
halisi ya kituo hicho.
Akielezea
hali halisi aliyoiona kituoni hapo, Profesa Muhongo alisema kwa wakati
huu kituo hicho cha Mtera hakizalishi umeme wa kiasi chochote huku
akitaja sababu kuwa ni upungufu wa maji uliosababishwa na matumizi
mabaya ya maji ya Bwawa hilo.
Profesa
Muhongo alisema njia bora ya utatuzi wa upungufu wa maji kwenye bwawa
hilo la Mtera ambalo hutumiwa na wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la
Umeme Nchini (Tanesco) kwa ajili ya kuzalisha umeme ni wadau kukaa
pamoja na kukubaliana namna ya kutumia maji hayo.
Mbali
na hilo, Profesa Muhongo alitaja utatuzi mwingine kuwa ni kuongeza
vyanzo vingine vingi vya kuzalisha umeme mbali na kutegemea maji ili
kuruhusu mabwawa hayo kufikia kina kinachohitajika.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akimsikiliza
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), Mhandisi
Felchesmi Mramba (kulia). Kushoto ni Meneja wa Kituo cha Kuzalisha Umeme
cha Mtera, Mhandisi Abdallah Ikwase.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akimsikiliza
Mwendesha mitambo ya Mtera, Cosbert Matandu (hayupo pichani). Kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba na katikati ni Meneja
wa Kituo cha Mtera, Mhandisi Abdallah Ikwase. Profesa Muhongo aliagiza
chumba cha kuendeshea mitambo ya kituo hicho kifungwe vifaa vya kisasa
ili kuboresha utendaji
Moja
ya Mtambo wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji wa Mtera wenye uwezo wa
kuzalisha Megawati 40 ukifanyiwa ukarabati. Ukarabati wa Mtambo huo
umeanza mwezi huu na unatarajiwa kukamilifika ifikapo mwezi Januari
mwakani.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akimsikiliza
mtaalamu kutoka Bodi ya Maji- Bonde la Rufiji, David Muginya (kulia)
akielezea kuhusu mikakati ya matumizi bora ya ili kuhakikisha kila sekta
inapata maji.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimsikiliza
Meneja wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Mtera, Mhandisi Abdallah Ikwase
akimuelezea kuhusu kupungua kwa kina cha maji kwenye bwawa la Mtera.
Muonekano wa Bwawa la Mtera kwa hivi sasa ikionesha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa kina cha maji.
No comments:
Post a Comment