Mshindi
wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Msimu wa nne Bi. Caroline Chelele
aliyekaa kwenye Pawatila akifurahia zawadi zake, Muda mfupi baada ya
kukabidhiwa.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Kilombelo Bw. Yahya Naiya (wa pili kushoto) aliye
muwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombelo akikata utepe kuashiria tukio la
kumkabidhi zawadi rasmi mama shujaa wa chakula msimu wa nne 2015 Bi.
Caroline Chelele, wa kwanza kushoto ni Mercy Minja Kaimu mkurugenzi wa
wa mji wa Ifakara, wa tatu kutoka kulia ni Mama Shujaa wa Chakula Bi.
Caroline Chelele na Mbunge wa Jimbo la Kilombelo Mh. Peter Lijuakali
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Kilombelo Bw. Yahya Naiya (wa pili kushoto) aliye
muwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombelo akimpongeza Mama shujaa wa
chakula 2015 baada ya kukabidhiwa zawadi ya vifaa vya kilimo vyenye
thamani ya Tsh Milioni Ishirini(20,000,000)
Vifaa
vya kilimo ambavyo alikabidhiwa mama Shujaa wa Chakula Msimu wa nne
2015, ikiwa ni Pawatila na Mashine ya kumwagilia na Shamba lenye Hekta 7
ambalo halipo pichani.
Mshindi
wa Shindano la Mama shujaa wa chakula linalo endeshwa na Oxfam kupitia
Programu yake ya Grow Bi Caroline Chelele akitoa neno la Shukurani baada
ya kukabidhiwa zawadi.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Kilombelo Bw. Yahya Naiya (wa pili kushoto) aliye
muwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombelo, akitoa neno la shukurani kwa
Shirika la Oxfam kwa jinsi wanavyo wajali na kuwawezesha wakulima wadogo
wadogo.
Mbunge
wa Kilombelo Mh. Peter Lijuakali akimpa pongezi mama shujaa wa Chakula
2015 kwa kuleta ushindi mkubwa wilayani hapo na kuwasihi akinamama
wengine wajitokeze kushiriki kipindi ambacho nafasi inatokea tena na
kurudisha ushindi huko.
Meneja wa Ushawishi na utetezi kutoka Oxfam Eluka Kibona akielezea kwa undani kuhusiana na shindano la Mama shujaa wa Chakula.
Mtaalam
wa Kilimo hai kutoka SOAM wa tatu kutoka kushoto akitoa maelezo ya
namna ya kutengeneza mbolea asiyo na kemikali yoyote kwa kutumia
Majani,Magugu, Majivu,Maji na Udongo
Baadhi ya wanakijiji wakifanya kazi kwa vitendo kwa kusombelea nyasi kavu pamoja na magugu kwa ajili ya kutengeneza Biwi
Shamba darasa la utayarishaji wa Biwi likiwa linaendelea
Baadhi ya wanakijiji ambapo mama Shujaa wa Chakula alipokabidhiwa zawadi zake, wakifuatilia kwa makini shamba Darasa
Mshindi
wa shindano la Mama Shujaa wa chakula 2015 msimu wa nne Bi. Caroline
chelele (Kulia) akimkabidhi zawadi Kaimu Mkurugenzi wa Mji wa Ifakara
Bi. Mercy Minja kwa niaba ya Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombelo
Bi.Caroline
chelele akikabidhi zawadi yake ya Kigoda kwa Shirika la Oxfam, kutoka
kushoto ni Narsis Silvesti, Eluka Kibona na wa kwanza kulia ni Suhaila
Thawer wote kutoka Oxfam Tanzania
Mama Shujaa wa chakula akikabidhi zawadi ya Picha kwa Shirika la Oxfam
Watalam
wa Kilimo hai kutoka SOAM wakimkabidhi vipeperushi vinavyozungumzia
kilimo hai Mama Shujaa wa Chakula 2015 Bi. Caroline Chelele
Baadhi ya wananchi waliokuwa katika sherehe hizo za kukabidhiwa zawadi mama shujaa wa Chakula.
Picha ya pamoja ya viongozi wa Wilaya ya Kilombelo, Shirika la Oxfam na
Mshindi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Msimu wa nne 2015
Bi.Caroline Chelele
……………………………………………………………………………………………….
Mshindi
wa shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015, Linaloendeshwa na Shirika
la Oxfam kupitia program yake ya Grow msimu wa nne Caroline Chelele
amekabidhiwa zawadi ya vifaa vya kilimo vyenye thamani ya kiasi cha
shilingi Millioni 20, nyumbani kwake kata ya Ifakara mkoani Morogoro.
Akizungumza
katika hafla ya makabidhiano hayo ya zawadi Mkoani Morogoro wilayani
Kilombero kata ya Ifakara,Meneja Ushawishi na Utetezi kutoka Shirika la
Oxfam,Eluka Kibona alisema zawadi hiyo ni moja ya utekelezaji wa
shindano hilo kwa mshindi aliyeshinda shindano hilo la Mama shujaa wa Chakula 2015.
Alisema
shirika lao linatoa takribani Milioni 20 kwa mshindi ambapo mshindi
anatakiwakuchagua zawadi ya vifaa vya kilimo ili kuweza kumuwezesha
zaidi. Kibona alisema Mshindi huyo alikabidhiwa Pawatila kwa ajili ya
kubebea Mazao,vifaa vya umuagiliaji pamoja na Shamba lenye Ekali 7.
“Huu
ni muendelezo wa shindano la mama shujaa wa Chakula kukabidhi zawadi
kwa ajili ya kuwainua wakulima wadogo wadogo kuonekana na Serikali kama
wao wanamchango mkubwa kwa jamii
kutokana na Chakula wanacholima ndicho kinacholisha taifa,”alisema Kibona . Aliongeza shindano hilo lipo chini ya Kampeni ya GROW yenye lengo la kuwainua wakulima wadogo wanaokumbana na changamoto mbalimbali katika kilimo.
kutokana na Chakula wanacholima ndicho kinacholisha taifa,”alisema Kibona . Aliongeza shindano hilo lipo chini ya Kampeni ya GROW yenye lengo la kuwainua wakulima wadogo wanaokumbana na changamoto mbalimbali katika kilimo.
Kwa
Upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero , Yahya Naniya
aliishukuru shirika hilo kwa hatua ya kuwathamini na kuwapigania
wakulima wadogo ambao asilimia kubwa kati yao ni wanawake.Alisema
kupitia shindano hilo linaweza kuongeza Chachu kwa wakulima kufanya
shughuli za kilimo kwa kasi na kuongeza wigo mpana wa kupata mazao mengi kutokana na Mashirika mbalimbali kuwawezesha.
kupitia shindano hilo linaweza kuongeza Chachu kwa wakulima kufanya
shughuli za kilimo kwa kasi na kuongeza wigo mpana wa kupata mazao mengi kutokana na Mashirika mbalimbali kuwawezesha.
Naye
Mshindi wa Shindano hilo 2015,Caroline Chelele alisema atahakikisha
zawadi hizo anazifanyia kazi ipasavyo itakayomuwezesha kumuongezea mazao
mengi zaidi. Aliomba Serikali pamoja na mashirika mbalimbali kuendelea
kuasidia wakulima wadogo na kuhakikisha nao
wanathaminiwa kama wakulima wakubwa.
wanathaminiwa kama wakulima wakubwa.
No comments:
Post a Comment