Mganga
Mkuu wa Jiji la Arusha, Dk Bakari Salum akifungua mkutano wa Wasaa wa
Mazingira (Earth Hour City Challenges) kwa watumishi wa halmashauri ya
Jiji la Arusha unaowajengea uwezo kuweka mipango inayoendana na
mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika kwenye hotel ya Palace jijni Arusha
kushoto ni Mratibu wa mradi wa nishati wa shirika la Utunzaji wa
mazingira duniani(WWF- Tanzania)Dk Teresia Olemako.
Mratibu
wa mradi wa nishati wa shirika la Utunzaji wa mazingira duniani(WWF-
Tanzania)Dk Teresia Olemako akizungumza kwenye mkutano wa Wasaa wa
Mazingira(Earth Hour City Challenges).
Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa Jiji la Arusha, Nteghenjwa Hoseah akiwasilisha
mada ya namna Jiji hilo lilijipanga kuhakikisha linakua safi kwa
kushirikiana na wadau na kulifanya kuwa kivutio cha watalii na wegeni
wengine.
Watumishi
wa halmashauri ya Jiji la Arusha wakifatilia kwa makini mada zilizokuwa
zikitolewa zenye lengo la kulifanya Jiji kuwa la mfano barani Afrika.
Afisa Mawasiliano wa WWF, Michael Bwoma (kushoto) akifatilia kwa makini wengine ni waandishi wa habari mkoani Arusha.
KUPIGA PICHA NA KOMBE LA BARCLAYS PREMIER LEAGUE KESHO LITAKUWA IPP MEDIA, MLIMANI CITY, MAZESE NA BIAFRA
Mkuu
wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Barclays hapa nchini, Osca Mwakyusa
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na
ratiba ya kutembeza Kombe la Ligi kuu ya Uingereza limeanza kutembezwa
jijini Dar es Salaam kuanzia leo Disemba 3, mwaka huu
Na kesho wapenzi
wa soka na ligi kuu ya Uingereza waombwa kujitokeza kwaajili ya kupiga
picha na kombe hilo ambalo limeaanza kutembezwa leo asubuhi. Ikiwa kwa
kesho asubuhi Kombe hilo litaanzia katika tawi kuu la benki ya Barclays
lililopo Posta na kuelekea katika ofisi za IPP Media na baadae Mlimani
City ambapo litakaa kwa muda wa lisaa limoja na baadae Kinondoni
Biafra, Mazese na kumalizia viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Meneja wa Bidhaa wa benki ya Barclays, Valence Luteganya.
Meneja
wa Bidhaa wa benki ya Barclays, Valence Luteganya kulia akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza kwa
wananchi kuwa Kombe la Ligi kuu ya Uingereza kuanza kupiganalo picha kwa
wapenzi wa soka jijini Dar es Salaam. Pia aliwasihi wananchi kufungua
akaunti za mshahara katika benki ya Barclays ili waweze kujishindia
tiketi mbili (2) za kwenda kuangalia soka la ligi kuu ya Uingereza bila
gharama yoyote kwa kuwa gharama zote zitakuwa zimelipiwa na benki hiyo.
Kuanzia kulia ni Mkuu wa mtandao wa matawi wa banki ya Barclays,
Emmanuel Katuma, Mkurugenzi wa kitengo cha wateja binafsi Benki ya
Barclays, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Barclays hapa nchini, Osca Mwakyusa.
Wafanyakazi
wa Benki ya Barclays hapa nchini wakipiga picha ya pamoja na kombe la
ligi kuu la Uingereza leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment