Maofisa kutoka Serikali ya Japan. |
Mazungumzo yanaendelea. |
Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akikabidhi zawadi ya picha kwa Waziri wa Nchi wa Mambo ya Nje wa Japan. |
Balozi Mahiga akiagana na Mgeni wake. |
TAARIFA
FUPI YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI,
KIKANDA NA KIMATAIFA KUHUSU UHUSIANO KATI YA JAPAN NA TANZANIA TAREHE 15
DESEMBA 2015
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga amefanya mazungumzo leo na
Waziri wa Nchi wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. Seiji Kihara ambaye
aliwasili nchini jana kama Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Japan Mhe.
Shinzo Abe ambapo kesho tarehe 16 Desemba 2015 anatarajiwa kuwasilisha
Ujumbe wa Waziri Mkuu wa Japan kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Joseph Magufuli.
Pamoja na kuwasilisha ujumbe kwa Mheshimiwa Rais, mgeni huyo anatarajiwa kuhudhuria hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mkopo wa dola za kimarekani milioni 96 utakaotolewa na Serikali ya Japan kwa
ajili ya mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirishia umeme wa Kenya na
Tanzania wenye urefu wa kilometa 441.5 kutoka Singida na Manyara kupitia
Babati na Arusha mpaka Namanga.
MAHUSIANO KATI YA TANZANIA NA JAPAN
Tanzania
na Japan zimekuwa katika uhusiano na ushirikiano wa karibu mara tu
baada ya Tanzania kupata uhuru wake. Mahusiano hayo yamekuwa yakikua na
kuimarika miaka hadi miaka katika nyanja mbalimbali ikiwemo miundombinu,
afya, nishati, Kilimo, biashara, viwanda, usafirishaji na uwekezaji.
Kufanyika kwa ziara hii ya Waziri wa Nchi wa Mambo ya Nje wa Japan ni
muendelezo wa kukuza ushirikiano baina ya nchi zetu mbili.
MIRADI MIPYA ITAKAYOFADHILIWA NA SERIKALI YA JAPAN
Serikali
imeingia makubaliano na Serikali ya Japan kutekeleza miradi mitatu ya
ujenzi wa barabara yenye lengo la kupunguza tatizo la msongamano wa
magari jijini Dar es Salaam linaloathiri uchumi wa nchi yetu. Miradi
hiyo ni pamoja na:
Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Juu katika eneo la TAZARA (TAZARA flyover):
Mkataba
wa ujenzi wa Barabara hiyo tayari ulikwishasainiwa tangu tarehe 15
Oktoba 2015 na ujenzi unategemewa kuanza mapema mwakani.
Mradi ya Ujenzi wa Barabara ya Morocco – Mwenge
Serikali
ya Japan itafadhili upanuzi wa barabara ya Mwenge – Morocco ili kuweza
kupunguza msongamano wa magari. Upanuzi wa barabara hii nao unatarajiwa
kuanza mwakani. Tayari Serikali imekwishaanza hatua za mwanzo za
ujenzi wa barabara hiyo kufuatia uamuzi wa Mhe. Rais kuelekeza fedha
zilizokuwa zigharamie sherehe za uhuru zitumike kuanza kazi ya upanuzi
wa barabara hiyo.
Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Gerezani mpaka bendera tatu
Mradi
huu unatarajiwa kutekelezwa kwa fedha za msaada kutoka Serikali ya
Japan. Ujenzi wa barabara hii nao unatarajiwa kuanza mwakani.
Mbali
na miradi ya ujenzi wa barabara, Serikali ya Japan imeingia makubaliano
na Serikali ya Tanzania kutekeleza miradi ya umeme kwa lengo la
kuongeza uzalishaji wa umeme wa kutosha kwa matumizi ya wananchi na
viwandani kama ilivyoahidiwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM. Miradi
itakayotekelezwa kwa ufadhili kutoka Japan ni pamoja na:
Mradi ya Ujenzi wa Njia ya Kusafirishia Umeme Kenya – Tanzania Power Interconnection Project
Mradi
huu una lengo la kuimarisha usambazaji kwa kuuza na kununua umeme
katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki hasa Kenya. Ni ujenzi wa njia
ya kusafirishia umeme wenye KV400 na urefu wa kilomita 414.5 kutoka
Singida na Namanga kupitia Babati na Arusha.
Mkataba
wa mradi huu unatarajiwa kutiwa saini baadaye leo Wizara ya Fedha na
kushuhudiwa na Waziri wa Nchi wa Mambo ya Nje wa Japan.
Ujenzi wa mradi wa Mtambo wa kuzalisha umeme katika eneo la Kinyerezi (Kinyerezi II power plant project).
Mkataba
wa ujenzi wa Mitambo ya kuzalisha umeme wa MW 300 huko Kinyerezi
ulisainiwa tarehe 27 Machi 2015 kati ya Serikali na Benki ya Kimataifa
ya Ushirikiano wa Kimaendeleo ya Japan (Japan Bank for International
Cooperation – JBIC). Utekelezaji wa Mradi huu unatarajiwa kuanza mapema
mwakani.
No comments:
Post a Comment