KAMPUNI YA TINGATINGA IMEINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA BRICOLEUR HOLDINGS Co.LIMITED YA JAPAN. - LEKULE

Breaking

16 Dec 2015

KAMPUNI YA TINGATINGA IMEINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA BRICOLEUR HOLDINGS Co.LIMITED YA JAPAN.



Mkurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan, Bi. Yu Shiran (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu kushirikiana kufanya kazi za sanaa na Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga, leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Sanaa Tingatinga, Bwana Zachi Chimwanda na kushoto ni Mkurugenzi pia wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan, Bwana Shoji Tsuchiya.
Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bwana Godfrey Mngereza akiwa na wanakikundi cha Sanaa cha Tingatinga na wajapani wakonyesha vibao vilivyochorwa na kikundi cha Sanaa cha Tinga Tinga jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bwana Godfrey Mngereza (kushoto) akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kusaini Mkataba wa makubaliano kati ya Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga na Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan. Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan Bwana Shoji Tsuchiya pamoja na Bi. Yu Shiran. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan Bwana Shoji Tsuchiya (kulia) wakibadilishana mikataba na kupeana mikono na Mwenyekiti wa Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga, mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika wa mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Japan Bi. Yu Shiran. 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwasikiliza na wakati wa kusaini wa Mkataba wa Makubaliano ya kufanya kazi na Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga na Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan uliofanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO)

CHAMA Cha Wasanii wa uchoraji picha aina ya Tingatinga imeingia mkataba wa miaka tano (5) na kampuni ya Bricoleurholdings Co.Limited ya nchini Japan, kwa ajili ya kuwatafutia soko nchini Japan 
Makabidhiano ya Mkataba huo yamefanyika leo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. 
Mwakilishi wa Kampuni ya Bricoleurholdings Co.Limited, Shoji Tsuchiya amemkabidhi mkataba huo Mwenyekiti wa Chama Cha Tingatinga, Zack Chimwanda, amesema kuwa kazi hii ya uchoraji wa picha aina ya Tingatinga imeanza nchini Tanzania ikiwa na mwanzilishi wake Edward Said Tingatinga ambaye alifariki dunia mwaka 1970 na jina la hilondipo lilipopatikana kutokana na yeye. 
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Hakimiliki Nchini (Cosota) Doreen Sinane,amesema kuwa kampuni ya BricoleurholdingsCo,Limited itakuwa inafanya kazi ya kuuza na kutafuta soko la picha zinazotengenezwa na wanachama wa Tingatinga. 
Kwa upande wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Ngereza, amesema kuwa sanaa ya uchoraji ni kazi kama kazi nyingine pia ni biashara inayomfanya msanii kupata kipato pamoja na kuliingizia taifa mapato.

No comments: