Mkurugenzi
wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini
Tanzania, Peter Malika akizungumza na wageni waalikwa wakati wa
makabidhiano ya misaada kwa miradi ya maendeleo iliyodhaminiwa na UNCDF
Tanzania.
Naibu
Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba akisoma hotuba yake wakati
wa kukabidhi hundi kwa mashirika binafsi na ya umma kwa ajili ya
kuendeleza miradi ya maendeleo.
Naibu
Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba (katikati) akimkabidhi hundi
bilioni moja na milioni sabini (1,070,000,000) Mkurugenzi wa Mji wa
Kibaha, Bi. Jennifa C. Omolo (kulia) na kushoto ni Mkurugenzi wa Mfuko
wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini Tanzania,
Peter Malika.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Moshi, Bw. Jeshi Godfrey Lupembe (kushoto) akikabidhiwa
hundi ya shilingi milioni mia tano na tisa (509,000,000/=) na Naibu
Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba (kulia) pamoja na Mkurugenzi
wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini
Tanzania, Peter Malika.
Naibu
Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba pamoja na Mkurugenzi wa
Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini
Tanzania, Peter Malika wakiwakabidhi masisita hundi ya milioni miamoja
na saba (107,000,000/=) wa kwanza kulia ni Msimamizi wa Mradi wa Umeme
wa Lupali, Sister Imakulata Mlowe na Sister Helga Silinu ambaye ni fundi
umeme katika mradi wa Lupali.
Mkuu
wa wilaya ya Ileje , Mh. Rosemary Senyamule (kulia) akipokea hundi ya
milioni mia mbili na milioni ishirini na sita (226,000,000/=) kutoka kwa
UNCDF iliyotolewa na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Tamisemi,
Kagyabukama E.Kiliba pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo
wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiendelea kufuatilia kwa makini kinachozungumzwa na baadhi ya viongozi.
Mkurugenzi
wa Mji wa Kibaha, Bi. Jenifa C. Omolo akitoa neno la shukrani kwa niaba
ya sekta za umma na sekta binafsi zilizopata msaada huo ili kuendeleza
miradi ya maendeleo hapa nchini.
Picha ya pamoja.
Na Mwandishi wetu
MFUKO
wa Maendeleo ya Mtaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) umetoa msaada wa
shilingi bilioni 2.4 kama kianzio cha mtaji kwa waandaaji wa miradi
kutoka sekta binafsi na umma. Katika
hafla iliyofanyika leo na kufunguliwa na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI,
Kagyabukama Kiliba hawala sita zilikabidhiwa wawakilishi wa waendeshaji
katika miradi iliyotawanyika sehemu mbalimbali nchini.
Pamoja
na hawala hizo za bilioni 2.4 imo pia shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya
miradi yenye mwelekeo wa kibiashara inayoandaliwa na mamlaka za
serikali za mitaa nchini Tanzania. Miradi
iliyopewa kianzio cha mtaji ni pamoja na halmashauri ya mji wa Kibaha
kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha basi na soko la kisasa, halmashauri ya
manispaa ya Moshi kwa ajili ya kituo cha kisasa cha mabasi cha biashara
na manispaa ya Ileje kwa ajili ya ujenzi wa mnara wa redio kwa
kushirikiana na sekta binafsi.
Mradi
mwingine ni wa uzalishaji wa umemejua (mtandao wa vijijini)
unaotekelezwa wilaya ya Korogwe na kampuni binafsi ya Ensol, mradi
binafsi wa uzalishaji umeme kwa maji unaoendeshwa na wanawake wa wilaya
ya njombe vijijini na mradi mdogo binafsi wa uzalishaji umeme wa Maguta
uliopo wilayani Kilolo. Akizungumza
kumkaribisha mgeni rasmi kutoa hundi hizo, Mkuu wa UNCDF nchini Tanzania
Peter Malika alisema msaada uliotolewa umelenga kuonesha mafanikio ya
program ya mradi wa fedha za nahalia (LFI) wa UNCDF katika kusaidia
waandaaji wanaojishughulisha na miradi inayotoa mchango katika maendeleo
ya uchumi ya maeneo husika.
“Licha
ya kuongezeka kwa upatikanaji wa mtaji wa uwekezaji kutoka vyanzo vya
umma na binafsi kwa ajili ya miundombinu, ni kiasi kidogo sana
kinachofikia miundombinu ambayo inaunda uti wa mgongo wa michakato ya
uchumi. LFI ilibuniwa ili kushughulikia changamoto hizi na uliundwa ili
kuonyesha kwamba miradi ya miundombinu ambayo inapewa kipaumbele na
serikali za mitaa na jamii inaweza kuvutia fedha endapo matatizo ya soko
la mtaji yaliyopo yatashughulikiwa” alisema Malika.
Aidha
Malika alisema katika mwaka huu timu ya LFI ilitoa msaada wa kiufundi
wa kulenga na kianzio cha mtaji kwa zaidi ya miradi 30,tisa kati ya hiyo
ikiwa katika hatua za juu na kwa hiyo kuwa tayari kupokea uwekezaji
ikiwemo miradi tisa iliyotunukiwa msaada jana. Tangu
kuanzishwa kwake mwaka 2012 LFI-T imesaidia zaidi ya miradi ya
maendeleo ya mahalia 30 nchini Tanzania katika hatua mbalimbali tangu
uwekaji mipango hadi kuwa tayari kupokea uwekezaji kwa kufanyakazi kwa
karibu na Tamisemi na taasisi za fedha.
Aidha
LFI-T inasaidia miradi katika mikoa 18 iliyo katika sekta mbalimbali
ikiwamo ya usindikaji mazao ya kilimo, tabia nchi, nishati salama na
uzalishaji wa bidhaa za viwandani. Naye
Naibu Katibu Mkuu Kiliba akizungumza na hadhara kabla ya kutunuku
hawala hizo sita alisifu kazi ya ubunifu iliyofanywa na UNCDF katika
utoaji fedha kwa maendeleo ya jamii na kusema hiyo ndiyo njia sahihi ya
kusababisha maendeleo. Pia
aliwapongeza waanzishaji wa miradi walipookea kianzia cha mtaji wa
uwekezaji kutoka UNCDF na kuwatakia mafanikio mema huku akisema kwamba
serikali ya Tanzania inakaribisha uendelezwaji wa program ya
LFI-Tanzania.
Kiliba
alisema kwamba wizara yake imeanzisha kitengo maalumu cha kuhakikisha
kwamba miradi ya ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi katika
halmashauri inafanikiwa.Mmoja wa
wakurugenzi wa halmashauri waliopewa mtaji huo wa kianzio, Jenifa Omolo
kutoka halmashauri ya mjui wa Kibaha alishukuru UNCDF kwa kufanikisha
halmashauri ya Kibaha kuwa na soko la kisasa na kituo cha basi cha
kisasa.
AlisemaUNCDF
na Tamisemi wamekuwa mstari wa mbele katika kuwezesha kutekelezwa kwa
wazo hilo kuanzia mwanzo hadi sasa wanapopata mtaji huo. Alihimiza
halmashauri nyingine nchini kupata msaada wa kiufundi kwa mawazo yao
kutoka UNCDF ili kuwa na uwezo wa kusimamia maendeleo ya umma na jamii. “Hatuna
soko katika mji wetu, kuna magenge tu na tuna kituo kidogo tu cha
mabasi ambacho hakikidhi mahitaji- hizi zimekuwa changamoto kubwa kwetu
kwa zaidi ya miaka kumi. Mji wetu unakua na sasa tunahitaji kuwa na
miundombinu ya kisasa” alisema Omolo na kuongeza kuwa mji wa Kibaha una
wajibu wa kutoa huduma bora na kwamba miundombinu mipya na ya kisasa
itasaidia kuongeza mapato kwa mji huo.
No comments:
Post a Comment