Msemaji
wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Ahmed Olotu (mzee Chilo)
akisoma waraka wa kupinga uamuzi wa Rais wa Shirikisho hilo Simon
Mwakifwamba kwa kutogombea tena nafasi ya Urais wa Shirikisho hilo
katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Ukumbi wa Idara ya
Habari (MAELEZO). Kushoto ni Mzee Ramadhani Ditopile.
Mzee
wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Hamisi Kagaye (kushoto)
akichangia mada wakati wa kupinga uamuzi wa Rais wa Shirikisho hilo
Bwana Simon Mwakifwamba wa kutogombea tena nafasi ya Urais wa Shirikisho
hilo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Ukumbi wa Idara
ya Habari (MAELEZO) leo. Kulia ni Mzee Ramadhani Ditopile.
Mmoja
wa wazee wanaounda Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Bi. Salome
Nonge (kulia) akichangia mada wakati wa kupinga uamuzi wa Rais wa
Shirikisho hilo Bwana Simon Mwakifwamba wa kutogombea tena nafasi ya
Urais wa Shirikisho hilo katika Mkutano na Waandishi wa Habari
uliofanyika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kushoto ni Mzee
Ramadhani Ditopile na Mzee Ahmed Olotu maalufu kama mzee Chilo.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wakifuatilia tamko la Wazee wa Shirikisho la
Filamu Tanzania (TAFF) lililohusu kupinga uamuzi wa Rais wa Shirikisho
hilo Simon Mwakifwamba wa kutogombea tena nafasi ya Urais wa Shirikisho
hilo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Ukumbi wa Idara
ya Habari (MAELEZO).
Na Skolastika Tweneshe na Tupokigwe Marco.
WAZEE
wa shirikisho la filamu Tanzania (TAFF) hawajakubaliana na uamuzi wa
Rais wa shirikisho hilo Bw. Simon Mwakifwamba kutogombea tena nafasi ya
Urais katika shirikisho hilo.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa wazee wa
Shirikisho hilo Bw. Ahmed Olotu maarufu kama Mzee Chilo amesema kuwa wao
kama Wazee wakongwe katika Shirikisho hilo wamemuomba Rais huyo agombee
tena wadhifa huo kwa mara nyingine ili aweze kumalizia mambo muhimu ya
maendeleo katika tasnia ya sanaa.
“Sisi
kama wasanii na Wazee wakongwe katika tasnia hii, bila kushurutishwa na
mtu yeyote tunapinga uamuzi wake wakutotaka kugombea tena nafafasi hiyo
.” Alisema Olotu.
Aidha,
ameongeza kuwa, miradi kama TAFF Trust Fund, TAFF Creative Ltd na
mingine mingi yenye kuhitaji umakini ambayo imehasisiwa chini uongozi
wake inahitajika kumaliziwa kwani bado haijakamilika.
Kwa
upande wake Bi. Salome Nonge (Mama Abdul) ameeleza kuwa, Bwana
Mwakifwamba ndiye aliyesaidia kupatikana kwa Ofisi ya Wasanii pamoja na
usafiri katika kazi zao.
“Binadamu hakosi kasoro ila kwa Mwakifwamba ni ndogo mno sasa hatutaki mtu mwingine aje.”Bi Salome alisema.
Naye
Bi. Salumu Ally (Mkasi) ameeleza kuwa uongozi wa Mwakifwamba umesaidia
wasanii kupata haki zao kama hati miliki zilizowezesha kupata maendeleo
ya kiuchumi kupitia sanaa wanaoifanya.
Hata
hivyo sanaa ya filamu inakuwa kwa kasi nchini pamoja na changamoto
zilizopo ambapo juhudi katika kutengeneza kazi zenye ubora zitakazoleta
ushindani katika soko la kitaifa na kimataifa bado zinahitajika.
No comments:
Post a Comment