MHAGAMA: AZITAKA HAMASHAURI ZOTE NCHINI KUTEKELEZA MAELEKEZO YA SERIKALI YA KUJIAANDAA NA KUKABILI MAAFA - LEKULE

Breaking

17 Dec 2015

MHAGAMA: AZITAKA HAMASHAURI ZOTE NCHINI KUTEKELEZA MAELEKEZO YA SERIKALI YA KUJIAANDAA NA KUKABILI MAAFA

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), akiangalia Sehemu ya mtaro wa maji katika eneo la Tegeta, Basihaya wilayani Kinondoni, Jijini Dar es Salaam leo wakati alipofanya ziara kuangalia jinsi wilaya hiyo ilivyojiandaa kukabili maafa ya Mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), akimsikiliza mkazi wa Tegeta, Basihaya Jijini Dar es Salaam, Jumanne Malongo alipokuwa akimueleza jinsi wembamba wa mtaro huo unavyosababisha maji kujaa katika makazi yao, leo wakati alipofanya ziara kuangalia jinsi wilaya hiyo ilivyojiandaa kukabili maafa ya Mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda. 
 Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Manisipaa kinondoni, Ando Mwakunga akimueleza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), uharibifu wa “kalvati” katika eneo la Boko, Ununio Jijini Dar es Salaam, leo wakati Waziri huyo alipofanya ziara kuangalia jinsi wilaya hiyo ilivyojiandaa kukabili maafa ya Mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), akiteta na Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya juu ya ujenzi wa mtaro wa maji katika eneo la Mnyamani, Buguruni wilayani Ilala, Jijini Dar es Salaam leo wakati alipofanya ziara kuangalia jinsi wilaya hiyo ilivyojiandaa kukabili maafa ya Mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo. 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), akitoa maelekezo baada ya kutoridhishwa na ujenzi wa mtaro wa maji katika eneo la Mnyamani, Buguruni Ilala Jijini Dar es Salaam, kwa Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo kumpatia taarifa ndani ya siku tano inayoeleza ni jinsi gani watakavyokamilisha ujenzi huo, leo wakati alipofanya ziara kuangalia jinsi wilaya hiyo ilivyojiandaa kukabili maafa ya Mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo.
 (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).

No comments: