Rais
Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi
wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU ambao
walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za
nje kwa watumishi wa umma.
Watumishi
hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas
ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka
kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi.
Agizo
hilo la Rais Magufuli lilitolewa jana na Balozi Mkuu Kiongozi Ombeni
Sefue wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari.
Balozi
Sefue amewataka watumishi wengine wa umma kutii agizo la Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kuonya kuwa
atakayekiuka atachukuliwa hatua kali.
No comments:
Post a Comment