Katibu
mkuu ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI)
Bwana Jumanne Sagini amemsimamisha kazi mkurugenzi wa halmashauri ya
wilaya ya Babati mkoani Manyara Mhandisi Mussa Natty ambaye (Pichani)
kabla ya kuhamishiwa wilayani Babati alikua mkurugenzi wa manispaa ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Bwana
Sagini amefafanua kuwa pamoja na kusimamishwa kazi, Mhandisi Natty
anapaswa kurudi katika halmashauri ya manispaa ya Kinondoni na kusubiri
uchunguzi zaidi dhidi ya tuhuma zinazomkabili.
Ametaja
tuhuma hizo kuwa ni pamoja na usimamizi mbaya uliosababisha barabara za
manispaa ya Kinondoni kujengwa chini ya kiwango na kutowachukulia hatua
watendaji wa manispaa waliokua chini yake, ukosefu wa uadilifu katika
ubinafsishaji wa eneo la ufukwe wa bahari la Coco Beach na malalamiko ya
wananchi juu ya viwanja katika eneo la Kinondoni ulioambatana na
usimamizi duni wa watumishi hasa wa sekta ya mipango miji na ardhi.
No comments:
Post a Comment