Afisa
Masoko wa Alaf, Theresia Mmasy akizungumza na waandishi wa habari
(Hawapo pichani)jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwandishi wa kitabu
cha Kolonia Santita,
Enock Maregesi na Mwandishi wa Ushairi la Kifaurongo, Christopher Budebah.
Mkuu
wa Idara ya Fasihi ya Mawasiliano na Uchapishaji (TATAKI) WA wa chuo
kikuu cha Dar es Salaam akiwa na baadhi ya viongozi ya ALAF Limited.
Mshiriki
wa Taaluma ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa, Adrian
Mtembei akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Mwandishi
wa kitabu cha Kolonia Santita, Enock Maregesi akipokea ua kutoka kwa
Mkurugenzi wa mabati ya Rolling Mills Kenya Sarit Shah leo wakati wa
kuwapongeza washindi wa uanishi wa fasihi za kiswahili Afrika.
Mwandishi
wa kitabu cha Kolonia Santita, Enock Maregesi akizungumza na waandishi
wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na tuzo aliyoipata katika
uandishi wa wa kitabu cha Kolonia ya Santita.
Mwandishi wa Ushairi la Kifaurongo, Christopher Budebah akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi.
KWA
mara ya kwanza Lugha ya Kiswahili imeingia katika rekodi ya dunia kwa
watanzania wanne kuchomoza katika tuzo ya waandishi ya Fasihi Afrika.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mshiriki wa Taaluma ya
Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa, Adrian Mtembei amesema
lugha ya Kiswahili ya kujivunia kutokana na watanzania wenye lugha yao
kuwa washindi.
Washindi
wa tuzo hizo ni Enock Maregesi ambaye aliandika Kolonia
Santita,Chiristophee Bubebah, Anna Manyaza aliandika Penzi la Damu,
Mohamed Ghassani aliandika N’na Kwetu.
Walioshiriki
katika tuzo hiyo walikuwa 65 na kuweza kuibuka watu wanne ambao ni
washindi wakitokea nchini na sherehe hizo zilifanyika Nchini Kenya.
Amesema
kwa lugha ya kifaransa na Kiingereza zimekuwa zikijitokeza kila mwaka
kwa watu kuandika riwaya na mashairi lakini Kiswahili imekuwa
ikisahaulika hivyo na kufanya Chuo Cornell Nchini Marekani iliamua
kufanya hivyo kuwa watu kuandika Riwaya na Mashairi.
Katika
tuzo hizo Kampuni ya watengenezaji wa Mabati ya Alaf ilizamini tuzo
hizo na kutaka watu wajitokeze katika kuinua lugha ya Kiswahili duniani.
Afisa
Masoko wa Alaf, Theresia Mmasy amesema kazi wataendelea kushirikiana na
watanzania katika kukuza Kiswahili katika kudhamini tuzo hizo.
No comments:
Post a Comment