SHIRIKA
la ndege la Etihad, ndege rasmi ya taifa za Falme za kiarabu na
Cognizant (NSADAQ: CTSH), shirika linaloongoza kwa huduma za teknolojia
ya habari, ushauri na biashara, leo wametangaza makubaliano ya kimkakati
yatakayoendesha mabadiliko ya kidijitali pande zote za shirika hilo
pamoja na washirika wake.
Chini
ya mpango wao wa miaka mitatu wenye thamani ya mamilioni ya madola,
Cognizant watawasaidia Etihad kufafanua mkakati wao wakidigitali na
kutengeza dhana mpya ambayo itatumika katika kutoa huduma bora kwa
wageni wao watakaosafiri popote na ndege za Etihad.
Kwa
kuleta pamoja mikakati ya kidijitali, teknolojia, sekta na uzoefu wa
ubunifu, Cognizant watafanya utafiti wa hali ya sasa ya biashara na
teknolojia ya shirika la ndege la Etihad na kutumia utafiti huo
kutengeneza mazingira ya kidijitali ya kiwango cha hali ya juu,
itakachowezesha usambazaji kupitia idhaa nyingi, ugawaji wa wateja kwa
kina zaidi na kubinafsisha ujuzi katika masoko.
Kwa
kutumia taarifa mbalimbali na ufahamu wa mteja, Cognizant italiwezesha
shirika la ndege la Etihad na washirika wake, kuelewa zaidi mahitaji ya
wageni wake.
Kwa
kuunganisha tafiti hizi na mazoea bora, michakato na teknolojia, shirika
hilo litawapa wageni wake suluhisho, ofa zitakazoendana na kila mteja
kwa mapenzi yake na itaboresha huduma zinazotolewa katika safari nzima
kutokana na hali ya uaminifu wao na upendeleo wa mteja kama vile bidhaa
na huduma, kuchagua wapendapo kukaa wakati wa safari, chaguo la mlo,
safari kipindi cha sikukuu na kadhalika. Kwa shirika hili, hii
inamaanisha kufungua mitiririko mipya ya mapato, kuongeza chapa na
kutengeneza fursa nyingine za kibiashara.
Afisa
Mkuu wa Biashara wa shirika la Etihad Peter Baumgartner, alisema,
“Wageni wetu wamezidi kugeukia idhaa za kidijitali zaidi kujiunga nasi
na hivyo tunatambua umuhimu wa kuwafikishia ubora wa kipekee na usio wa
dosari katika sehemu zote tunazofikia.
Ushirikiano wetu na Cognizant utatusaidia kufikia kiwango bora katika safari za kidijitali ambayo itawaburudisha wateja kuanzia kupanga safari hadi kununua tiketi, kwenye uwanja wa ndege na kwenye ndege, na itaboresha uaminifu wa wageni kwa kuwavutia na kuwashirikisha wageni katika njia mpya na za kisasa.”
Ushirikiano wetu na Cognizant utatusaidia kufikia kiwango bora katika safari za kidijitali ambayo itawaburudisha wateja kuanzia kupanga safari hadi kununua tiketi, kwenye uwanja wa ndege na kwenye ndege, na itaboresha uaminifu wa wageni kwa kuwavutia na kuwashirikisha wageni katika njia mpya na za kisasa.”
Robert
Webb ambae ni Afisa Mkuu Habari na Teknolojia wa shirika la Ndege la
Etihad, alisema “Ushirikiano huu ni muhimu kwa mikakati yetu teknolojia
na uvumbuzi ambayo hutuimarisha na washirika wetu katika kujipanga upya
kuwapatia wageni wetu huduma bora katika safari zao ambayo inaendana
wakati wa safari na tamati yake.
Tumechagua Cognizant kwa sababu wanaongoza katika programu za kidijitali, uzoefu wa kidigitali kwenye huduma za usafiri, ukarimu na ushirikiano wa muda mrefu na shirika na pia ni viongozi katika dunia ya teknolojia.”
Tumechagua Cognizant kwa sababu wanaongoza katika programu za kidijitali, uzoefu wa kidigitali kwenye huduma za usafiri, ukarimu na ushirikiano wa muda mrefu na shirika na pia ni viongozi katika dunia ya teknolojia.”
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Cognizant, Francisco D’Souza, alisema: “Tumefurahia
kushirikiana na Etihad kutengeneza shirika la ndege lenye kuwapa kilicho
bora wateja wake wakati wa safari zao kwa kutumia nguvu ya teknolojia
ya kisasa. Kwa Cognizant, mfumo wa kidijitali’ inamaanisha kuwa na uwezo
wa kuunganisha teknolojia, takwimu za kisayansi, vifaa, ubunifu na
mikakati ya kibiashara kubadili mifumo na uzoefu.
Ushiriki
huu unaweka alama ya kuungana kwa mashirika mawili yenye kasi ya
uongozi ambayo mikakati yao ya ukuaji inabebwa na uvumbuzi wa
kidijitali. Timu ya kazi za kidijitali ya Cognizant inafurahia na
kutegemea mengi kwa kusaidiana na shirika la ndege la Etihad pamoja na
washirika wake ikiwemo kuleta udhibiti, urahisi na uwazi kwa msafiri wa
kisasa.
Muamko
wa kidijitali utazidi kuimarisha shirika la Etihad katika kuwa na chapa
yenye kiwango cha hali ya juu kwa kutoa huduma bora kwa wateja.
Kama
sehemu ya ushirikiano huu, Cognizant itasimamia program za Etihad na
kuziunganisha katika jukwaa jipya la kidijitali. Kituo cha ubora wa
kidijitali itaanzishwa kuendesha uvumbuzi pamoja na washirika wakuu wa
kiteknolojia wa Etihad.
No comments:
Post a Comment