Mwenyekiti
wa bodi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Ramadhani Dau akikata utepe
kuashiria uzinduzi wa ofisi mpya kwenye ghorofa ya pili ya jengo la
benki hiyo lililopo jengo la Makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es
Salaam leo. Katikati ni Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays
Tanzania, Kihara Maina akiwa na baadhi ya wadau wa benki hiyo wakati wa
kuzindua ofisi ya benki hiyo ghorofa ya pili ya benki hiyo.
Mwenyekiti
wa bodi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Ramadhani Dau akifungua
kitambaa kuashiria uzinduzi wa ofisi ya benki hiyo katika jengo la
benki ya Barclays ghorofa ya pili leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akishuhudia wakati akifungua kitambaa hicho.
Mkurugenzi
mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akizungumza
na wafanyakazi wa benki ya Barclays hapa nchini (hawapo pichani) leo
jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Barclays hapa nchini wakimsikiliza Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina.
Baadhi ya wanabodi ya benki ya Barclays wakimsikiliza Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina mara baada ya kuzindua ofisi mpya leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment