Afisa
Elimu Vifaa na Takwimu Halmashauri ya Kibaha Vijijini Doris Semkiwa
ambaye anamwakilisha Afisa Elimu wa Halmashauri ya Kibaha Vijijini
akitoa mada kwa Washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Walimu na
Wanafunzi katika Ufundishaji na Ujifunzaji kwa shule za sekondari (STEP)
wakifuatilia mafunzo hayo katika kituo cha Shule ya sekondari
Kilangalanga iliyopo wilayani Kibaha Vijijini mkoani Pwani.
Washiriki
wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Walimu na Wanafunzi katika Ufundishaji
na Ujifunzaji kwa shule za sekondari (STEP) wakifuatilia mafunzo hayo
katika kituo cha Shule ya sekondari Kilangalanga iliyopo wilayani Kibaha
Vijijini mkoani Pwani.
Washiriki
wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Walimu na Wanafunzi katika Ufundishaji
na Ujifunzaji kwa shule za sekondari (STEP) ambao wanafundisha somo la
Biolojia wakitafuta baadhi ya sampuri za kufundishia somo hilo kulingana
na mazingira waliopo. Mafunzo hayo ni ya siku tano kuanzia Tarehe
Disemba 19 hadi 23, 2015 katika kituo cha Shule ya sekondari
Kilangalanga iliyopo wilayani Kibaha Vijijini mkoani Pwani.
Baadhi
ya sampuri zilizokusanywa na washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo
Walimu na Wanafunzi katika Ufundishaji na Ujifunzaji kwa shule za
sekondari (STEP) kwa ajili ya kufundishia la Biolojia kulingana na
mazingira waliopo.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO).
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Walimu
nchini wametakiwa kuwa wazalendo kwa kuhakikisha wanawafundisha
wanafunzi katika muda waziada ili kuwaongezea uwezo wa ufaulu katika
mitihani yao.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Bw. Zuberi Samataba
wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Walimu na wanafunzi katika
ufundishaji na Ujifunzaji kwa shule za sekondari (STEP) yanayoendelea
katika mikoa sita nchini.
Aidha,
Bw. Samataba aliwataka walimu wasihangaike kutafuta michango kwa ajili
ya uendeshaji wa shule na badala yake wajikite katika kufundisha na
kuwasaidia wanafunzi kupata elimu na kufaulu masomo yao kwa kuwa
Serikali ndiyo itafanyakazi ya kuhakikisha fedha za uendeshaji wa shule
na vifaa vinapatikana kwenye shule zote za Serikali nchini.
Mafunzo
hayo ni ya siku tano (5) ambayo yanashirikisha walimu wa shule za
sekondari wapatao 2,528 yameanza kufanyika kuanzia Desemba 19, 2015 na
yanatarajia kumalizika Desemba 23, 2015.
Mafunzo
hayo yanayolenga kuwajengea uwezo walimu na wanafunzi katika
ufundishaji na ujifunzaji yanafanyika kwa awamu ambapo katika awamu ya
pili yanafanyika katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Iringa, Singida
na Katavi na hatimaye kufanyika katika mikoa yote nchini.
Katika
awamu ya kwanza ya mafunzo ya STEP iliyofanyika mwezi Juni, 2015
ilishirikisha mikoa ya Mwanza, Dodoma, Geita, Mara, Simiyu, Shinyanga na
Tanga ambapo walimu wa sekondari wapatao 3,880 walipatiwa mafunzo hayo.
Katika
kila awamu ya mafunzo, walimu wane wa masomo ya Kiswahili, Hisabati,
Biolojia na Kiingereza kutoka kwenye shule za sekondari katika
Halmashauri na Mkoa husika wanashiriki katika mafunzo katika vituo
mbalimbali vinavyoandaliwa na mikoa husika.
Katika
mafunzo hayo, walimu wanajengewa uwezo wa kuwawezesha kuwatambua
wanafunzi wenye uwezo mdogo kimasomo na walio katika hatari ya kufeli
mitihani ya Taifa kwa kuwapatia mafunzo rekebishi kwa lengo la
kuwawezesha kufaulu mitihani yao.
Mafunzo
yanayotolewa ni sehemu ya utoaji wa mafunzo ya walimu kazini ikiwa ni
utekelezaji wa Programu ya kuboresha taaluma ya Walimu na Wanafunzi wa
shule za Sekondari ambayo ni mojawapo ya Mpango wa Tekeleza kwa Matokeo
Makubwa Sasa (BRN).
Programu
ya STEP ilibuniwa na Serikali kwa lengo la kubadilisha hali ya kushuka
kwa ufaulu wa wanafunzi na kuboresha kiwango cha ufaulu kwa kuwawezesha
walimu kujenga tabia ya kuwatambua wanafunzi wenye uwezo mdogo kimasomo
na walio katika hatari ya kufeli Mtihani wa Taifa kwa kuwasaidia kufanya
Mafunzo Rekebishi.
Ili
kuyafanya mafunzo ya nayotolewa kufanyika kwa ufanisi, Ofisi ya
Rais,TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
imeandaa miongozo ya masomo husika unaotumika kuwafundishia walimu hao.
Mafunzo
ya STEP yanatekeleza azma ya Serikali chini ya mpango wa BRN unaolenga
kuweka mfumo thabiti wa kusimamia, kufuatilia na kutathmini mipango yake
hususan Mpango wa Kupunguza na Kuondoa Umaskini Tanzania (MKUKUTA) na
Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.
BRN ni
mfumo ambao umejikita katika kuweka vipaumbele, kufanya ufuatiliaji
makini na uwajibikaji katika kuleta matokeo tarajiwa, Elimu ni mojawapo
wa sekta za kipaumbele katika utekelezaji wa BRN nchini.
Sekta
ya Elimu inavipaumbele tisa (9) vilivyoainishwa ambavyo ni upangaji wa
shule kwa ubora wa ufaulu katika matokeo ya mitihani ya kumaliza elimu
ya msingi na sekondari kidato cha nne, utaratibu wa utoaji tuzo kwa
shule zinazofanya vizuri ilikuzipamotisha wa kuendelea kufanya vizuri,
kuandaa kiongozi cha kuimarisha utendaji wa shule na kutoa mafunzo kwa
wakuu wa shule na kufanya upimaji wa stadi za Kuandika, Kusoma na
Kuhesabu (KKK) kitaifa.
Maeneo
mengine ya vipaumbele katika sekta ya elimu ni pamoja na kutoa mafunzo
ya Ufundishaji wa KKK kwa walimu wa darasa la kwanza na pili, kujenga
uwezo wa Walimu na wanafunzi katika Ufundishaji na Ujifunzaji, Ujenzi wa
Miundombinu muhimu ya shule, Utoaji wa Ruzuku ya Uendeshaji na Motisha
kwa walimu.
No comments:
Post a Comment