Van Gaal awawakia waandishi wa habari, sababu ipo hapa! - LEKULE

Breaking

25 Dec 2015

Van Gaal awawakia waandishi wa habari, sababu ipo hapa!

louis-van-gaal-press-conference

Kocha wa Manchester United, Louis Van Gaal (pichani) amewalalamikia waandishi wa habari kwa kuandika habari kuhusu yeye ambazo sio sahihi kuhusu hatma yake ndani ya Manchester United kutokana na matokeo mabovu wanayoyapata.
Van Gaal aliingia katika mkutano na wanahabari na kuanza kuzungumza kuwa wamekuwa wakiandika habari ambazo hazina ukweli ambazo zinakuwa hazipendezi kwa kuandika kitu kisicho sahihi na kudanganya wasomaji kuhusu hali halisi iliyopo.
“Mnatakiwa kuwa na maelezo yenye usahihi, nilipokuwa nikipokea simu kutoka Ed Woodward, Sir Alex Ferguson na David Gill sababu ya habari mnazoandika zinakuwa siyo nzuri, hilo halina uhalisia na sasa natakiwa kujibu maswali yenu lakini sidhani kama nahitaji kufanya hivyo”
Van Gaal akaulizwa swali kuhusu kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kusema maneno yanayosemwa kwa sasa kuhusu Van Gaal ni kumkosea heshima kocha huyo na akajibu kwa kuuliza kama kuna mwandishi hajihisi kuwa na hatia na anatakiwa kuomba msamaha kwake.
“Hakuna mtu kwenye chumba hiki anahisi kuomba msamaha kwangu? Hilo linanishangaza, ninafikiri kuwa nilifukuzwa, nililisoma hilo au nilifukuzwa, au mwanafunzi wangu [Jose Mourinho] amechukua nafasi yangu?,
“Mnafikiri hili linamtokea mke wangu au watoto wangu? au wajukuu wangu? au mashabiki wa Manchester United? au marafiki zangu? wananiita mara nyingi tunazungumza na ndiyo maana Arsene Wenger kasema hivyo,” alisema Van Gaal na kuongeza “Mnadhani nataka kuongea na vyombo vya habari kwa sasa? nipo hapa sababu ya sheria za ligi ninatakiwa kuongea na nyie lakini naona ninaloongea na nyie mnaliandika vile mnavyotaka nyie”

Baada ya kuzungumza kuhusu kukerwa kwake na vyombo vya habari, akazungumzia mchezo wao wa jumamosi siku ya kufungua zawadi “boxing day” dhidi ya Stoke City na kusema “Hatupo katika nafasi nzuri kwa wiki nne zilizopita, tulikuwa tukiongoza ligi na katika wiki nne mbele tunaweza kuwa katika nafasi nzuri”

No comments: