NIYONZIMA ATOA NENO KWA YANGA PAMOJA NA MASHABIKI - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Friday, 25 December 2015

NIYONZIMA ATOA NENO KWA YANGA PAMOJA NA MASHABIKI

Haruna

Haruna Niyonzima amewataka mashabiki wake kuwa wavumilivu kwani suala lake linatarajiwa kupatiwa ufumbuzi hivi karibuni baada ya kuwasilisha maelezo kwa uongozi wa timu yake.
Niyonzima pia ameitakia mafanikio mema timu yake katika mchezo wa Juamamosi itakapokuwa ikicheza dhidi ya Mbeya City.
“Yanga ni timu yangu na nimeishi nayo vizuri pamoja na watu wake, lakini sina furaha kuwa nimekaa nje kwa muda usiojulikana au kuwa pembeni ya timu lakini haya yote ni majaribu na najua ni vitu ambavyo vipo duniani ila naamini yataisha vizuri tu”, amesema Niyonzima.
“Mimi ni binadamu naweza kufanya makosa lakini nawahakikishia wapenzi wa Yanga na Niyonzima kwamba hili litaisha siku si nyingi na wataendelea kupata burudani kama ilivyokuwa au hata zaidi”.
“Tuna mechi Jumamosi na Mbeya City, nawatakia mechi nzuri na pia nawatakia wana Yanga Merry Christmas na Happy New Year. Tumalize mwaka 2015 kwa amani na tuanze mwaka 2016 kwa amani, kwa wapenzi wa Haruna pia kwa watanzania wote”.

Niyonzima amesimamishwa kwa muda usiojulikana na uongozi wa Yanga kutokana na kuchelewa kurudi kujiunga na timu hiyo mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Challenge Cup 2015 michuano iliyokuwa ikifanyika nchini Ethiopia ambapo yeye alikuwa akiitumikia timu yake ya taifa ya Rwanda na kuisaidia kufika hatua ya fainali lakini ilipoteza mchezo wa fainali mbele ya Ugando
Post a Comment