Ukataji
wa Utepe mwekundu (Kutoka kushoto kwenda kulia): Naser Al Mazroei,
Mkurugenzi mtendaji kitengo cha huduma kwa wateja katika mamlaka ya
vitambulisho Emirates; Ray Gammell, Afisa mkuu wa Utendaji na Watu
kutoka Shirika la ndege la Etihad; Dk Nadia Bastaki, Makamu rais huduma
za matibabu; Dk Mariam Buti Al Mazrouei, Kaimu afisa mtendaji wa
Ambulatory Healthcare Services; and Dk. Mubarak Al Darmaki, Kaimu afisa
mkuu wa kliniki kutoka Ambulatory Healthcare Services.
Shirika la
ndege la Etihad ambalo ndio shirika rasmi la nchi ya Falme za kiarabu,
leo hii imefungua milango ya kituo cha afya chenye hadhi ya kimataifa
kwa ajili ya wafanyakazi wake Abu Dhabi. Kituo hiki ambacho ni kikubwa
kwa mazingira kitatoa huduma za kliniki, huduma za kitabibu kwa
wafanyakazi wenye visa pamoja na raia wenye vitambulisho toka falme za
kiarabu.
Kituo hicho
kilichopo jengo la Etihad Plaza, mjini Khalifa, kitaruhusu wafanyakazi
zaidi ya 23,800 wa shirika hili la ndege wenye makazi nchi ya Falme za
kiarabu kupata huduma bora za kitabibu, katika mazingira ya kisasa
karibu kabisa na makao makuu ya shirika hilo la ndege.
Afisa mkuu
wa rasilimali watu na Utendaji, Ray Gammell, alisema “Kama muajiri bora
zaidi duniani, tunajivunia kwa kutoa huduma kwa timu yetu kubwa ya
wafanyakazi, wakiwemo wa nchi ya falme za kiarabu na wakigeni. Kituo
hiki kipya kitaruhusu tuendelee kuboresha programu zetu zinazolenga
kutunza afya za wafanyakazi wetu na hivyo kuongeza ufanisi wao wa kazi
Upanuzi wa
Kliniki mpya ya anga ni sehemu ya mkakati maalumu wa shirika la ndege la
Etihad kuwa na kituo cha afya kinachoongoza katika kanda hiyo. Kituo
kikiwa na wahudumu wa afya zaidi ya 30 waliobobea, wakiwemo madaktari
bingwa 10, vyumba sita vya uchunguzi, vyumba tisa vya madaktari na vifaa
vya kisasa kabisa kusaidia wafanyakazi, kliniki ina ahidi kutoa huduma
bora kabisa ya kitatibu na afya kwa wafanyakazi wa shirika la ndege la
Etihad.
Dk. Nadia
Bastaki, makamu raisi wa huduma za afya, alisema “Kliniki mpya yenye
viwango vya kisasa kabisa inaonyesha dhamira yetu kuendelea kutoa huduma
za afya zenye viwango vya juu kabisa kwa ajili ya wafanyakazi wetu
ikiwemo marubani na wahudumu wa ndani ya ndege. Kliniki hii inasimamiwa
na mamlaka ya afya ya Abu Dhabi (HAAD) na mamlaka ya usafiri wa anga UAE
(GCAA), tukiwa na furaha ya kutambulika kama moja ya kituo
kinachoongoza katika huduma za utabibu na vifaa katika sekta ya anga.”
Wafanyakazi
wa shirika la ndege la Etihad pamoja na wategemezi wao pia wataweza
kupata huduma kutoka kituo hiki cha matibabu ili kusaidia mchakato wa
maombi ya VISA. Kuna makubaliano yaliyosainiwa mwezi Februari 2015 na
Ambulatory Healthcare Services – SEHA kuendesha kituo hicho na kutoa
huduma za vipimo kwa ajiliya Visa kama X-Ray, vipimo vya damu na vipimo
vya mwili
Dk. Mariam
Buti Al Mazrouei, Kaimu mtendaji mkuu wa Ambulatory Healthcare Services
(AHS), alisema: “lengo letu kuu baina ya SEHA na AHS ni kuboresha
upatikanaji wa huduma za kiafya na ufunguzi wa kituo cha vipimo kwa
ajili ya mchakato wa VISA ni mfano wa jinsi gani lengo letu linaweza
kufikiwa kupitia ushirikiano wa wadau kutoka sekta mbalimbali nchini.
Kituo kipya kinaleta idadi ya vituo vinavyoendeshwa na AHS kufikia jumla
ya vituo kumi na moja, na hivyo kuimarisha nafasi yetu kama vinara
wakutoa huduma ya vipimo vya afya kwa ajili ya mchakato wa VISA kwa nchi
ya Falme za kiarabu”
Aidha kituo
cha mamlaka ya vitambulisho cha Emirate pia kikiwa kimejengwa eneo
husika ili kutoa huduma kwa wafanyakazi takribani 200 kupata
vitambulisho kila siku. Eneo husika litasaidia kupunguza kwa kiasi
kikubwa msongamano na mchakato mzima wa kupata vitambulisho vya Emirates
kwa wafanyakazi na wategemezi wao hapa nchi ya Falme za kiarabu.
Hapo
mbeleni kutakuwa na nafasi kwa raia wa Emirate kupata mafunzo na ujuzi
wa unesi kupitia mpango wa chuo cha mafunzo ya unesi cha Fatima,
kikilenga kuvutia manesi nchini humo kupata ajira katika sekta ya anga
pia.
Kituo kipya
kinafuatia utambulisho wa huduma ya ambulance kwa wafanyakazi, kliniki
maalumu kwa wanaosafiri kikazi, vituo kadhaa vya afya na mazoezi huko
Abu Dhabi pamoja na kituo mahususi kwa ajili ya kusaidia ustawi wa
marubani pamoja na wahudumu wa ndani ya ndege.
No comments:
Post a Comment