Serikali
ya Uturuki imeahidi kuisaidia Serikali ya Tanzania kufanikisha mpango
wa utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi utakaoanza January mwakani.
Hayo
yalizungumzwa jana na Balozi wa Uturuki nchini Bi Yasemin Eralp
alipokuwa akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt Tulia Ackson Mwansasu alipomtembelea ofisini kwake.
Balozi
yasemin Eralp aliainisha Serikali ya Uturuki imekuwa ikisaidia
Tanzania katika miradi mbalimbali nakuwa na ushirikiano wa Mabunge ya
nchi hizo mbili ambao umeongeza mahusianio mazuri ya nchi hizo, mbali na
ushirikiano wa Bunge ameweka wazi kuwa serikali yake ya Uturuki
inaweza kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuwezesha miradi ya
maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, ujenzi wa maktaba za shule,ujenzi
wa viwanda na ujenzi wa vituo vya Afya na Hospitali nchini.
“Katika
kuunga mkono mpango wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
kutoa elimu bure kwa watanzania kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari
tuko tayari kushirikiana na serikali kwa kutoa msaada wa vifaa kwa
wanafunzi kama vile vitabu, kompyuta na kujenga maktaba katika shule
mbalimbali”alisema Balozi Eralp.
Naye
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia
Ackson Mwansasu aliishukuru Serikali ya Uturuki kwa kusaidia Tanzania
katika miradi ya kimaendeleo na kuzidi kuomba ushirikiano zaidi toka
kwao hasa katika maswala ya Bunge katika nchi hizo.
“Tunaishukuru
Serikali ya Uturuki kwa ushirikiano wao katika maswala ya Bunge na
kujenga mahusiano mazuri na Tanzania na hata katika miradi ya maendeleo
ya jamii inayofadhiliwa na serikali ya Uturuki na tunaomba tuendeleza
mahusiano zaidi katika mahusiano ya mabunge ya nchi hizi mbili ” alisema Dkt Tulia.
Tanzania
imekuwa na mahusiano mazuri na Uturuki katika maswala ya Bunge na mwaka
2010 wawakilishi toka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya
aliyekuwa Spika wa Bunge hilo Mhe. Samwel Sitta walitembelea Bunge la
Uturuki kwa mwaliko wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Uturuki wakati huo
Mhe. Mehmet Ali Sahim.
No comments:
Post a Comment