CHAMA
cha Mawakala wa Forodha nchini (TAFFA) kimesema kuwa wizi wa kontena
bandari ya Dar es Salaam na kusababisha serikali kukosa mapato ni tatizo
la muda mrefu ambalo ni limekuwa likisababishwa na watumishi wa
bandari.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Rais wa TAFFA, Steven
Ngatunga alisema tatizo lilojitokeza ya uondoshaji wa kontena 329
katika bandari Kavu ya Azam ilitokana na baadhi ya watumishi wa baadhi
ya benki na Bandari kuingilia taarifa katika mfumo na kusababisha
serikali kukosa mapato.
Ngatunga
alisema kuwa tatizo la serikali kukosa mapato katika bandari ya Dar es
Salaam walishagundua lakini serikali ilishindwa kuchukua hatua mpaka
serikali ya awamu ya tano kugundua hilo na hatua zimechukuliwa kwa wale
waliohusika.
Alisema
TAFFA itatoa ushirikiano kwa kile ambacho wanakiona katika bandari ya
Dar es Salaam juu ya watu wanaosababisha serikali kukosa mapato kwa
maslahi yao binafsi.
Aidha
alisema kuwa kuna kampuni zilionekana kuwa zipo kwa ajili ya kukwepa
kodi ya serikali ambazo chama kiliona na kupeleka malalamiko ambayo
mwisho wa siku kukawepo urasimu wa kukutana viongozi ambao wanaweza
kushughilikia hilo.
Alisema
baadhi ya mawakala walilipia kontena lakini wanaambiwa malipo
hayakufanyika huku wakiwa na kumbukumbu za malipo na kusababisha kutilia
shaka juu ya uadilifu wa watumishi wa benki pamoja na bandari.
TAFFA
imesema haiko tayari kwenda na mawakala ambao wanaharibu taaluma hiyo
na kusababishia serikali kukosa mapato ambayo ndio ya kufanyia maendeleo
nchini.
Alisema
kuwa kuna kampuni 73 zimefungwa wakati hawahusiki katika uondoshaji wa
kontena katika bandari na bandari kavu kutokana na kampuni hizo kuwa
kulipia kontena zinazodaiwa kukwepa kodi.
No comments:
Post a Comment