Aliyekuwa
mgombea ubunge wa jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya CCM, Philemon
Mollel amepinga matokeo ya uchaguzi huo yaliyompa ushindi wa kishindo,
Godbless Lema wa Chadema.
Akiongea
na waandishi wa habari baada ya msimamizi wa uchaguzi huo kutangaza
matokeo, Mollel alidai kuwa kulikuwa na udanganyifu mkubwa ambao
unafanya matokeo hayo kutokuwa halali.
Alisema
kuwa wakati zoezi la kupiga kura likiendelea kuna gari lililokamatwa
likiwa na kura bandia za kumpa ushindi Lema ingawa alidai gari hilo
liliachiwa baadae.
“Kulikuwa
na Noah ya diwani wa Chadema ambayo ilipita katika baadhi ya vituo vya
kupigia kura na kudai kupeleka vyakula. Lakini gari hiyo tumeambiwa
ilikuwa na kura za bandia zilizofanikiwa kuingizwa kwenye
masanduku,”alisema Mollel.
Kadhalika,
alieleza kuwa kulikuwa na mapungufu makubwa kwenye fomu za matokeo kwa
kuwa baadhi ya fomu hazikuonesha idadi ya kura zilizopigwa.
Mollel alilirushia lawama jeshi la polisi kwa madai kuwa liliwatisha akina mama na wazee kwenda kupiga kura.
“Hakukuwa na vurugu zozote, kwanini kuwatishia wanachi kwa silaha na vifaa vya kivita,” alihoji Mollel.
Matokeo
yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi huo uliofanyika Jumapili,
Disemba 13 yalimpa ushindi Godlbess Lema kwa kupata kura 68,848 sawa na
asilimia 65.9 huku Philemon Mollel akipata kura 35,607 sawa na asilimia
34 ya kura zote halali zilizopigwa na kuhesabiwa
No comments:
Post a Comment