WAZIRI
wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora George
Simbachawene amewaagiza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurungenzi
wote wa halmashari nchini kuhakikisha wanazoa taka zote zilizokusanywa
wakati wa siku ya uhuru kabla ya tarehe 20 mwezi huu.
Kauli
hiyo aliitoa wakati alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo
wakati wa kikao cha kumkaribisha katika ofisi ya Tamisemi mjini
Dodoma.
Alisema
kuwa hataki kuona hadi ifikapo tarehe 20 ya mwezi huu kuwa uchafu wa
siku ya uhuru bado unaendelea kulalamikiwa na watu kuwa bado
haijaondolewa katika maeneo uliokusanywa.
“Hadi
ifikapo tarehe hiyo sitaki kusikia uchafu bado haujaondolewa katika
maeneo ulipokusanywa toka siku ya uhuru lakini pia unapoondolewa huo
kuna uchafu mwingine unakuja hivyo basi watendaji wanaohusika wa
hakikishe kuwa wanaanda maeneo ya kuupeleka” alisema Simbachawene.
Aidha
aliwataka watumishi wa Tamisemi kubadilika katika utendaji wa kazi zao
na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani awamu ya tano ya haitaendelea
kuwalea watendaji wavivu.
Kwa
upande wake,Naibu Waziri wa wizara hiyo Suleiman Jaffo, aliwataka
watumishi wa Tamisemi kubadilika katika utendaji wao wa zamani ili
waweze kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuweza kuboresha maisha ya
wananchi.
No comments:
Post a Comment