Mahakama
kuu ya Tanzania imeridhia dhamana kwa washitakiwa watatu wa mamlaka ya
mapato Tanzania TRA wanaokabiliwa na mashitaka ya kutoa makontena 329
bandarini bila kulipiwa kodi na kuisababishia serikali hasara ya
shilingi bilioni 12.7.
Maamuzi
hayo ya mahakama kuu ya Tanzania yametokana na ombi lililowakilishwa
mahakamani hapo na washtakiwa watatu wakiongozwa aliyekuwa Kamishina wa
Forodha wa TRA Bw Tiagi Masamaki.
Jaji
wa mahakama hiyo Bi Wilfrida Koroso, alisema dhamana kwa washitakiwa
hao watatu iko wazi kama watatimiza masharti sita yakiwemo ya kulipa
hundi ya shilingi bilioni 2.6 kila mmoja huku pia wakitakiwa kuwasilisha
hati zao za kusafiri na kutakiwa kuwa na wadhamini watakaokuwa na uwezo
wa kusaini hundi ya shilingi milioni 20 kila mmoja.
Mshitakiwa
namba moja katika kesi ya kuhujumu uchumi, aliyekuwa Naibu Kamishna wa
mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Tiagi Masamaki (Kulia) akiwa na
wenzake aliyekuwa Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Habibu
Mponezya na Bulton Mponezya wakiwa katika Mahakama Kuu Tanzania jijini
Dar es Salaam jana wakisomewa shtaka linalowakikabili la makosa ya
jinai na uhujumu uchumi.
No comments:
Post a Comment