Ujumbe
wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU EOM) kwa Tanzania
unatoa tena wito kwa ukamilishwaji haraka wa mchakato wa uchaguzi
Zanzibar kulingana na kanuni za chaguzi shirikishi, za uwazi,
zinazotekelezwa kwa wakati na za kuaminika.
Kufuatia
Siku ya Uchaguzi tarehe 25 Oktoba, Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa
Umoja wa Ulaya umebaki nchini kufuatilia chaguzi zilizoahirishwa
Tanzania Bara na mchakato uliyositishwa Visiwani Zanzibar, baada ya
tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) la tarehe 28
Oktoba, lililofuta matokeo ya uchaguzi mkuu Zanzibar.
EU
EOM ilikutana na wadau wakuu Visiwani, vikiwemo vyama vya siasa, Mwana
Sheria Mkuu wa Serikali wa zamani na wa sasa, wadau wa sharia na
mahakama, asasi za kiraia na maafisa uchaguzi. Bahati mbaya EU EOM
haikuweza kukutana na Mwenyekiti wa ZEC.
EU
EOM inafahamu kuhusu mazungumzo yanayoendelea kati ya CCM na CUF,
yanayowashirikisha Marais Wastaafu wa Zanzibar. EU EOM inarudia tena
wito uliyotolewa kwa pamoja na jumbe zingine za uangalizi za kimataifa
tarehe 29 Oktoba, unaoishauri ZEC kuonyesha uwazi kamili kufuatia uamuzi
wake wa kufuta uchaguzi na uongozi wa kisiasa Zanzibar kuweka maslahi
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar kwanza, kwa lengo la
ukamilishwaji haraka wa mchakato wa uchaguzi, kulingana na kanuni za
kidemokrasia za chaguzi pamoja na sheria za Zanzibar.
“EU
EOM imekuwepo nchini tangu 11 Septemba kufuatilia mchakato wa uchaguzi
ndani ya Muungano na Zanzibar. Idadi kubwa ya waangalizi 141 wa EU
nchini walirejea Ulaya katikati ya mwezi Novemba, lakini timu ndogo ya
watathmini wa uchaguzi ilibaki nchini kufuatilia ngazi zilizobaki za
mchakato wa uchaguzi,” alisema Muangalizi Mkuu wa EU EOM, Judith
Sargentini.
“Japokuwa
mchakato wa uchaguzi Zanzibar haujakamilika, EU EOM itarejea Ulaya kwa
muda tarehe 8 Desemba. Umoja wa Ulaya unaendelea hata hivyo, kuunga
mkono kikamilifu mchakato wa uchaguzi Zanzibar na kwa mchakato mpana
zaidi wa kidemokrasia Tanzania. EU EOM iko tayari kurejea na kuangalia
mchakato wa uchaguzi Zanzibar pindi makubaliano ya kuendelea na mchakato
huo yanayolingana na chaguzi shirikishi, za uwazi, zinazotekelezwa kwa
wakati na za kuaminika yatakapofikiwa,” aliongeza Muangalizi Mkuu.
EU
EOM ilitumwa kufuatia mialiko toka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar. EU EOM
inapenda kutoa shukrani zake kwa NEC kwa kuiongezea muda wake kupita
muda uliyopangwa awali, jambo linaloashiria upana wa wigo na mamlaka ya
EU EOM, ambayo yanahusisha zaidi ya uangalizi wa muda mfupi. Ujumbe
ulitoa tamko lake la awali la mchakato wa uchaguzi tarehe 27 Oktoba.
Tarehe
29 Oktoba, EU EOM, pamoja na jumba zingine za waangalizi za kimataifa
za Umoja wa Afrika, SADC na Jumuiya ya Madola, ilitoa tamko la pamoja
kuhus Zanzibar. EU EOM itawasilisha ripoti kamili ya kina, ikiwemo
mapendekezo kwa chaguzi zijazo, ndani ya miezi mitatu ya kukamilika kwa
mchakato wa uchaguzi.
No comments:
Post a Comment