KUNA
ule msemo wa watu wa mjini, kuwa "Uki-beep, napiga" na kweli leo hii
Desemba 8, 2015 umetokea pale Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA, barabara
ya Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam, mlipa kodi mmoja alitupia
ujumbe kwenye mtandao wa kijamii akiomba wataalamu wa IT wa TRA, wafike
haraka kwenye ofisi zao za TRA Barabara ya Samora kwani mitambo ya
ku-print Motor Vehicles License ime-collapse", na watu wamekaa tu
wasijue la kufanya.
ilichukua
kama dakika 15 au 20 hivi, watu wawili waliovalia suti maridhawa na
dada mmoja "aliyeshiba", walitinga kwenye ofisi hizo, na kukuta walipa
kodi wakiwa wamejazana kwenye mabenchi wakijipepea tu, kutokana na joto
kali.
Mmoja
wa watu hao waliovalia suti, alianza kuwauliza walipa kodi, "Jamani
vipi huduma za hapa mnaridhika nazo."? Aliuliza mmoja wao.
Walipa
kodi hao kwanza walimtazama, na mmoja "akajilipua", hapana haturidhiki
nazo, hapa unapotuona tumeshakaa sana, huduma hakuna tunaambiwa mtandao
haupo, tumeshindwa kuchapishiwa stika za malipo ya kodi ya barabarani.
Mwingine
akasema, hata hali ya hewa humu ndani kama unavyoiona joto kali, hakuna
viyoyozi, na tumekuja kulipa kodi hii ni sawa??, akahoji mlipa kodi
huyo.
Baada
ya majibu hayo, Mlipa kodi mmoja aliibuka na kuwaambia wenzake, jamani
semeni huyo ndiye bosi mpya wa TRA, "tiririkeni" yaani semeni, na hapo
malalamiko yakawa mengi, naye bosi huyo ambaye si mwingine bali ni Dkt.
Philip Mpango, ambaye hivi karibuni,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, alimteua kukaimu nafasi ya Kamishna
Mkuu wa TRA, akiziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Kamishna Rished
Bade, akawajibu, nimeyapokea malalamiko yenu, na ndiyo maana mmeniona
niko hapa, nilipokea ujumbe kutoka kwa mlipa kodi akilalamika kuwa hapa
kwenye tawi letu huduma zimesimama, nikaona nifike kujua nini kimetokea.
Alisema Dkt. Mpango akiwaambia walipa kodi hao ambao walionekana
kufurahishwa na maneno hayo.
Wakati
akiwaeleza hayo, mitambo hiyo ghafla ikaanza kufanya kazi na waliokuwa
jirani na madirisha walianza kuitwa mmoja mmoja na kupatiwa huduma.
Hiyo ndiyo serikali mpya ya awamu ya tano yenye kauli mbiu "Hapa Kazi Tu", hakuna kulala kila mtu anapiga kazi tu.
"figisu
figisu" ya kile wafanyakazi wa hapo waliwaambia wateja wao kuwa "system
iko down", yaani kwa maana ambayo wao wamezoea kuwaambia wateja kuwa
mtandao wa computer haufanyi kazi kwa hivyo walipa kodi kibao
waliokuwepo kwenye ofisi hizo, walilazimika kukaa tu kwenye mabenchi
wakimuomba mungu mtandao huo upone ili waweze kupata "stika" za magari
yaani Motor Vehicles License.
Pichani Dkt. Mpango (kushoto), akizungumza na walipa kodi hao kwenye tawi la TRA, barabara ya Samora Desemba 8, 2015.
No comments:
Post a Comment