Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akifungua Kikao Maalum
cha Wadau kutoka nje ya Magereza(hawapo pichani) cha kujadili rasimu ya
Mpango wa Jeshi la Magereza wa kujitosheleza kwa chakula cha Wafungwa
waliopo Magerezani. Kikao hicho kimefanyika leo Desemba 8, 2015 katika
Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
Mshauri
Mwelekezi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Beatus
Kundy(aliyesimama) akiwasilisha rasimu ya Mpango wa Jeshi la Magereza wa
kujitosheleza kwa chakula cha Wafungwa waliopo Magerezani. Jeshi la
Magereza limeandaa rasimu hiyo ili kuipunguzia Serikali gharama za
kuwalisha wafungwa waliopo magerezani.
Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa
Andiko hilo(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji,
Eng. Deonice Chamulesile(wa pili kulia) ni Kamishna wa Sheria na
Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kushoto) ni Kamishna wa
Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga.
Mwakilishi
kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Hashim Kimmwe akitoa
mchango wake wakati wa kujadili rasimu ya Mpango wa Jeshi la Magereza wa
kujitosheleza kwa chakula cha Wafungwa waliopo Magerezani.
Wataalam
wa Jeshi la Magereza walioshiriki kikamilifu katika maandalizi ya
Andiko la Mpango wa Jeshi la Magereza kujitosheleza kwa chakula kwa
kushirikiana na Mshauri Mwelekezi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
wakifuatilia majadiliano ya rasimu hiyo.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment