Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa vifaa mbalimbali
vitakavyotumika kuwahudumia wagonjwa katika hospitali hiyo.
Msaada
wa vitanda kumi utatumika katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU)
pamoja na wodi nyingine. Msaada huo umetolewa na Jumuiya ya Australia na
Tanzania.
Vifaa
vingine vilivyotolewa ni pamoja na Stretcher’ nne zitakazotumika
kusafirishia wagonjwa ambao hawawezi kukaa, kifaa cha kufanyia mazoezi
kwa wagonjwa na baiskeli ya magurudumu matatu.
Akipokea
msaada huo Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi katika hiyo Agness Mtawa
ameishukuru Jumuiya hiyo na kutoa rai kwa wadau wengine kuendelea kutoa
msaada katika hospitali hiyo.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa
Mseru akizungumza leo katika mkutano uliowajumuisha viongozi wa Jumuiya
ya Australia na Tanzania kabla ya hospitali hiyo kukabidhiwa vifaa vya
wagonjwa vikiwamo vitanda na baiskeli za magurudumu matatu.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Australia na Tanzania, Didier Murcia akimsikiliza Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Mseru leo wakati wa mkutano na
viongozi wa jumuiya hiyo na wataalamu wa hospitali hiyo. Kulia ni
Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk John Kimario wa MNH.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminieli Aligaesha
akiwa katika mkutano huo uliofanyika leo kabla ya kukabidhiwa kwa vifaa
vinavyotumika kuwasaidia wagonjwa wakati wa kupatiwa matibabu.
Mkurugenzi
wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Bi.
Agness Mtawa akipokea msaada wa vitanda na vifaa vingine leo kwenye
hospitali hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Australia na
Tanzania, Didier Murcia akimkabidhi Sister Mtawa vifaa hivyo na kulia ni
Mkurugenzi wa jumuiya hiyo, Thierry Murcia.
Mkuu
wa Idara ya Uuguzi na Mazingira ya Ndani, Bi. Zuhura Mawona akisalimiana
na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Australia na Tanzania, Didier Murcia kabla
ya kupokewa kwa msaada huo leo katika hospitali hiyo.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Australia na Tanzania, Didier Murcia akiwa katika picha
ya pamoja na wauguzi wa hospitali hiyo baada ya kukabidhiwa msaada huo
leo.
No comments:
Post a Comment