Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imelishukia Baraza Kuu la Waislamu Tanzania
kutokana na kuwepo ongezeko kubwa la maombi ya misamaha ya kodi.
TRA
imeiandikia Barua Bakwata baada ya kubaini kuwa kati ya mwaka 2006 na
Septemba mwaka huu, Baraza hilo limeingiza magari 82 yenye msahama wa
kodi.
Barua
hiyo ya TRA kwenda Bakwata iliyosainiwa na Meneja Misamaha ya Kodi wa
TRA, Mwamtum Salim inamueleza Katibu Mkuu wa Bakwata kuwa kutokana na
kuwepo ongezeko kubwa la maombi ya misamaha ya Kodi, Mamlaka hiyo
itaanza kufuatilia kwa ukaribu zaidi maombi hayo.
TRA
ilitoa siku saba kwa Baraza hilo kuhakikisha inawasilisha nyaraka
kadhaa ikiwa ni pamoja kuonesha safari za magari, bima, stakabadhi ya
mafuta, uthibitisho kuonesha fedha zilizonunua magari hayo pamoja na
kitabu cha mahesabu cha Taasisi hiyo.
No comments:
Post a Comment