Kaimu
Mkurugenzi Mkuu, Tume ya Nguvu za Atomiki, Tanzania, Dr. Mwijarubi
Nyaruba aliekaa katikati pamoja na wataalamu wa Shirika la Nguvu za
Atomiki Duniani katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya namna
ya kukabiliana na kuimarisha ulinzi wa matukio ya kinyuklia.
Tume
ya Nguvu za Atomiki, Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Nguvu za
Atomiki Duniani wanaendeshesha mafunzo ya namna ya kukabirina na matukio
ya mionzi hatari, mafunzo haya yatachukua siku nne na yameanza jana
jumatatu tarehe 07 disemba na yatafika ukomo wake tarehe 10 disemba,
2015, mafunzo haya yana jumla ya washiriki 23 kutoka katika nchi sita za
ukanda wa Afrika ikiwa ni Uganda, Kenya, Zimbabwe, Botswana, Ethiopia,
Namibia na mwenyeji Tanzania mafunzo yanalenga zaidi kutoa mwongozo
jinsi ya kukabiliana na majanga yanayoweza kusababishwa na mionzi hatari
ya nyuklia endapo hakutakuwa na uangalizi wa kutosha.
Akifungua
mafunzo haya jijini Arusha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za
Atomiki, Tanzania Dr. Mwijarubi Nyaruba amesema, kutokana na kukua kwa
kasi kwa teknolojia duniani ni muhimu sana kwa nchi wanachama wa shirika
la nguvu za atomiki duniani kuendelea kutoa mafunzo na kujadiliana
jinsi ya kukabiliana na majanga yanayoweza kusababishwa na mionzi
ayonisha.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu Dr. Nyaruba aliendelea kufafanua kuwa kutokana na
ongezeko la vitendo vya ugaidi duniani ni lazima kujiimarisha kwa namna
yoyote ile ili kuweza kulinda vyanzo vyote vya mionzi vinavyotumika
mahospitalini na sehemu zingine za viwanda pamoja na kuvitafuta vyanzo
vya mionzi ambavyo vimetekelekezwa au kupotea (Orphan Sources) na
kuvihifazi kwa umakini mkubwa vyanzo hivi hatari, visijie kuingia katika
mikono ambayo sio salama na kutumika katika matukio ya kigaidi na
kuleta athari kubwa kwa wananchi pamoja na mazingira kwa ujumla, hivyo
ni jukumu la nchi wanachama kuendelea kubadilishana uzoefu ili kuweza
kuzibiti vyanzo hivi.
Naye
mshiriki kutoka Kenya , ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha kuzuia
majanga, ndugu Pius Masai Mwachi amesema kuwa ni muda muhafaka sasa kwa
nchi zote za jumuhiya ya afrika mashariki kukaa pamoja na kutafuta
suluhisho la namna ya kukabiliana na majanga yote yanayoweza
kusababishwa na mabaki ya mionzi, kwani mionzi ni hatari sana na ni
lazima kama nchi wanachama hasa waheshimiwa maraisi wa nchi hizi za
jumuhiya ya adfrika mashariki kuweza kuhakikisha wanatoa kipaumbele
kikubwa ili kuweza kukabiliana majanga yanayoweza kusababishwa kwa
kutumia mabaki ya mionzi.
Mtaalamu
mshiriki kutoka Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani IAEA Ndugu John
Jones amesema kuwa dunia kwa ujumla inakabiliana na changamoto kubwa juu
ya matukio mbalimbali ya kigaidi yanayoendelea duniani, hivyo Nchi zote
wanachama ikiwepo Tanzania wana jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa juhudi
kubwa zinafanyika ili kuweza kukabiliana na hari yoyote hatarishi pindi
matukio na majanga ya kinyuklia yanapoweza kutokea.
Tanzania
Kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki imejenga jengo maaalumu la kuhifadhia
mabaki ya mionzi Central Radioactive Waste Management Facility (CRWMF)
ambapo vyanzo vyote vya mionzi vilivyokwisha nguvu kutoka mahospitalini,
sehemu za tafiti pamoja na viwandani huchukuliwa na kusafirishwa kwa
umakini mkubwa na kuhifadhiwa katika jengo hilo maalumu.
No comments:
Post a Comment