Marehemu Hellen Stephen Mbebha wakati wa uhai wake.
Spika
wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) akiweka shada la maua juu ya
kaburi la aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi Shughuli za Bunge Marehem Hellen
Mbebha.
Katibu
wa Bunge la Tanzania Dkt. Thomas Kashilillah akitoa heshima za mwisho
kwa kwa mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi Shughuli za Bunge Marehem
Hellen Mbebha ambapo mazishi yake yalifanyika katika kijiji cha
Kung’ombe wilayani Bunda mkoa wa Mara tarehe 01/12/2015. Aliyesimama ni
Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge Bi. Nenelwa Wankanga.
Makamishna
wa Tume ya Utumishi wa Bunge Mhe. Kangi Lugola na Mhe. Abdulkadir Shah
wakiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Hellen Mbebha.
Watoto wa marehemu Helen Mbebha, Nassoro na Nasra, wakiwa na Babu na Bibi yao wakati wa mazishi ya mama yao kipenzi.
Mama
mzazi wa marehemu Hellen Mbebha akiwa hajiwezi wakati wa kuusindikiza
mwili wa binti yake makaburini huko Wilaya ya Bunda kijiji cha
Kung’ombe.
Mhe. Rose Kamili (Mb) akiongoza wabunge wanawake kuweka shada la maua juu ya kaburi la marehemu Hellen Mbebha.
Hii
ndyo ilikuwa safari ya mwisho ya marehemu Hellen Mbebha hapa duniani.
BWANA alitoa, BWANA alitwaa. Jina la BWANA na lihimidiwe. Amina (Picha
na Prosper Minja – Bunge)
No comments:
Post a Comment