Wananchama na viongozi wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa mjini
Morogoro wamefanya sherehe zenye lengo la kumuombea hekima na uvumilivu
aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa.
Taarifa
kutoka mjini Morogogoro zinaeleza kuwa sherehe hizo nusura zivunjike
baada ya kutawaliwa na majonzi kwa hali ya juu huku baadhi ya
wahudhuriaji wakidondosha machozi kutokana na maelezo yaliyokuwa
yakitolewa na viongozi wa vyama hivyo.
Mmoja kati ya waandaaji wa
sherehe hizo, Bi. Bertha Kombe alieleza katika sherehe hizo kuwa vijana
wengi walitupa kadi zao za kupigia kura baada ya matokeo ya urais huku
afya za akina mama wa chama hicho zikidhoofu kutokana na kutoridhishwa
na muenendo wa uchaguzi huo.
“Vijana wengi mitaani wamevunjwa
mioyo na kutupa shahada zao za kupigia kura, kina mama tumejikuta
tukikonda na kushindwa kula kwa sababu tunatumia muda mwingi kutafakari
kilichotokea,” alisema Bi. Kombe.
Viongozi wa Chadema waliwashukuru wananchi kwa kuitikia wito na kuwataka kuanza harakati za kuomba kura kwa ajili ya mwaka 2020.
No comments:
Post a Comment