Diamond Platnumz alikuwepo, Kampala, Uganda usiku ambao Zari alikuwa
akifanya party yake ya All White lakini hakutokea. Ex wa Zari, Ivan
Ssemwanga na wapambe wake walikuwepo.
Watu walihisi kuwa Diamond
aliogopa kwenda kumpa kampani mama wa mtoto wake Tiffah ili kuepusha
shari na kambi ya Rich Gang ya Ivan.
Hata hivyo muimbaji huyo wa Utanipenda amedai kuwa hakukacha party
hiyo bali makubaliano aliyokuwa nayo na promota wa show yake ya Ijumaa
(siku moja baada ya all white party) yalimtaka asiende kwenye show hiyo
ili kutengeneza uspesho kwenye show yake na Patoranking na sio ukweli
kuwa alimgwaya Ivan.
“Halafu sasa watu wanasema namuogoa [Ivan], mimi siwezi kumuogopa,
hii code chafu kabisa kutoka Tandale mimi nimuogope mtu!,” alisema
kwenye mahojiano ya jana kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.
Diamond amesema ameshawahi kukutana na Ivan mara kibao japo walipigiana mikausho kama kawa!
“Sijawahi kuwa na matatizo naye, nshakutana naye wakati naenda kwenye
MTV alikuwepo, mara nyingi tulikuwa tunapishana hivi na hivi kabisa.
Hatujawahi kusalimiana sababu sijawahi kuwa na mahusiano naye niseme
nimsalimie ni uongo. Halafu nilikuwa nikipita, nipo na crew, security,
yeye anakuwa anapita tu maskini ya Mungu.”
No comments:
Post a Comment