Miongoni mwa maswali mengi ambayo yanaendelea kuulizwa kuhusiana na utaratibu mpya wa vyombo vya habari kuanza kuwalipa wasanii kwa kucheza nyimbo zao kuanzia mwakani, ni pamoja na kiasi gani msanii atakuwa analipwa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Hakimiliki Tanzania (Cosota), Doreen
Sinare alisema kuwa wanamuziki, watunzi na maproducer watalipwa
asilimia 60 kwa kila wimbo au video itakayochezwa katika redio na
televisheni yoyote ndani na nje ya nchi kwa kutumia vifaa bora
vilivyowekwa na kampuni ya CMEA.
Doreen alisema kuwa mwanamuziki, msanii alitakiwa kupata asilimia 70
ya kazi yake, lakini asimilia 10 itakatwa katika malipo hayo na kuingia
katika mifuko ya jamii kwa mahitaji yake ya baadaye.
Alisema kuwa wanamuziki ni sawa na wafanyakazi wengine na asilimia 10
hiyo itamwezesha kujipatia kipato chake kama ilivyo kwa wafanyakazi
wengine katika taasisi mbalimbali.
COSOTA kwa kushirikiana na kampuni ya kusimamia kazi za wanamuziki
nchini Copyrights Management East Africa Limited (CMEA) wataanza kulipa
mirabaha ya wanamuziki na wadau wake kuanzia mwakani.
No comments:
Post a Comment