Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinafanyia kazi uteuzi wa Katibu
Mkuu wa chama hicho kufuatia aliyekuwa Katibu Mkuu wake, Dk. Willbrod
Slaa kujivua wadhifa huo baada ya kujitoa kwenye siasa za vyama.
Pamoja
na kutokuwa tayari kumtaja mrithi wa Dk. Slaa, Mwenyekiti wa CHADEMA,
Freeman Mbowe anatarajiwa kuteua jina la mwananchama ambaye atashika
wadhifa huo.
Katika
majina yanayochomoza miongoni mwa wana-CHADEMA kushika mikoba hiyo ni
jina la Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu, Frederick Sumaye na
aliyekuwa mgombea mwenza wa CHADEMA, akiungwa mkono na UKAWA, Duni Juma
Haji maarufu kama "Babu Duni'.
Duru
za kisiasa zinaeleza kuwa uamuzi wa hivi karibuni wa Frederick Sumaye
kujiunga na CHADEMA ni moja katika mchakato mzima wa kumwezesha
kuteuliwa kushika nafasi hiyo ya juu katika utendaji katika CHADEMA.
Chama
hicho kinaona haja ya kumpa wadhifa huo Sumaye ili aendelee kuwepo
katika medani za kisiasa na hivyo kumweka katika haiba nzuri ya
kuendelea kuwa mpiga debe wa CHADEMA katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020
na chaguzi zote ndogo zitakazojitokeza kufuatia rufani za wagombea
ubunge wa CHADEMA waliokata rufaa kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu
uliofanyika okroba 25, 2015.
Kwa
upande wa Duni Juma Haji, ambaye awali alisemekana kuwa na mpango wa
kurudi CUF ambako anadaiwa kuwa na kazi maalum, ameendelea kuwepo
CHADEMA kimahesabu kwa matarajio kwamba endapo Seif Sharrif Hamad
atafanikiwa kuwa Rais wa SMZ basi Babu Duni atafaa kuwa Katibu Mkuu wa
CHADEMA ili kudumisha mahusiano kati ya CHADEMA na CUF.
Hili
nalo limekaa katika mfumo ule ule wa mahesabu ya kisiasa kwani CHADEMA
wanamwona Babu Duni kuwa ni mtaji wa uhusiano huo kati ya vyama hivyo
vikuu vya upinzani nchini ambapo mtaji huo utwawezesha CHADEMA kuingia
Ikulu ya Magogoni katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
No comments:
Post a Comment