Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete atunukiwa Heshima ya Companion Award na Commonwealth Partnership for Technological Management (CPTM) - LEKULE

Breaking

5 Dec 2015

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete atunukiwa Heshima ya Companion Award na Commonwealth Partnership for Technological Management (CPTM)

Taasisi ya Commonwealth Partnership for Technological Management (CPTM) inayojishughulisha na kukuza ushirikiano katika nyanja ya sayansi na teknolojia kwa nchi za Jumuiya ya Madola, imemtunuku Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, heshima ya Juu ya CPTM (Companion Award) kwa kutambua mchango wake katika kuhamasisha ukuaji wa matumizi ya sayansi na teknolojia ikiwemo matumizi ya huduma za fedha kwa njia ya simu.
 
Rais Mstaafu Kikwete, alikabidhiwa Tuzo hiyo tarehe 1 Desemba, 2015. 
 
Taasisi hiyo yenye makao makuu yake London ndio inayoendesha Midahalo ya Kimataifa maarufu kama Smart Partnership Dialogue.
 
 Mkutano wa mwisho wa aina hiyo ulifanyika Dar es Salaam mwaka 2013 ukiwa Na kali mbiu ya "Kutumia Teknolojia Kuchochea Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii Barani Afrika". 
 

Rais  Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Cheti cha Kumtunuku Yeshima ya Juu ya CPTM (Companion Award). Aliyesimama kushoto kwa Rais Mstaafu ni Dkt. Tan Sri Omar, Mwenyekiti wa Bose ya Wakurugenzi wa CPTM na pembeni yake ni Dkt. Mihaela Smith, CEO wa CPTM. Tuzo hiyo imetolewa wakati wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPTM ambao uliambatana na maadhimisho ya Miaka 20 ya Taasisi hiyo jijini London
 


Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akitoa neno la shukurani baada ya kutunukiwa tuzo ya  heshima ya Juu ya CPTM (Companion Award) wakati wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPTM ambao uliambatana na maadhimisho ya Miaka 20 ya Taasisi hiyo jijini London.

No comments: