Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI akagua hali ya mazingira ya soko la Temeke Sterio, jijini Dar - LEKULE

Breaking

5 Dec 2015

Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI akagua hali ya mazingira ya soko la Temeke Sterio, jijini Dar

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Bw. Zuberi Samataba (aliyetangulia) akikagua machinjio ya kuku jana katika soko la Temeke Sterio Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Bw. Photidas Kagimbo (wa pili kushoto) akimwongoza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Bw. Zuberi Samataba(katikati) kukagua soko la Temeke Sterio lililopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.Zoezi hilo lilifanyika jana wilayani humo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la usafishaji wa mazingira.
Katapila la Halmashauri la Manispaa ya Temeke likizoa uchafu jana katika soko la Temeke Sterio ikiwa ni utekelezaji agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la usafishaji wa mazingira.
Takataka zikiwa zimezagaa mitaani baada ya kutupwa na wananchi wa Kiburugwa katika Manispaa ya Temeke.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Bw. Zuberi Samataba(kulia) akitoa agizo kwa Mkuu wa Idara ya Usafishaji na Manispaa ya Manispaa ya Temeke Bw. Ally Hatibu ya kuondoa mara moja uchafu katika eneo la barabara ya Kiburugwa ambayo wakazi wa huko wamegeuza sehemu ya kutupa takataka. Agizo hilo alilitoa jana wakati alipofanya ziara ya kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la usafishaji wa mazingira.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Bw. Zuberi Samataba(katikati) akitoa mwongozo jana juu ya suala la kufanya usafi kwa wakuu wa idara(hawapo pichani) wa Halmashauri wa Manispaa ya Temeke. Wengine katika picha ni Mkurugezi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Bw. Photidas Kagimbo (kushoto) na Mkurugenzi wa Utumishi na Raslimali Watu wa TAMISEMI Bw. Mohamed Pawaga(kulia).

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Bw. Zuberi Samataba akisisitiza juu ya utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la usafi wa mazingira ,jana wakati alipotembelea Ofisi ya Msimamizi wa soko la Temeke Sterio lililopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke. Picha zote na Beatrice Lyimo -MAELEZO 

No comments: