MANISPAA
ya Ilala kwa kushirikiana na ForumCC wako katika hatua za mwisho za
uanzishaji wa Mfuko wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi ukiwa na
lengo la kukusanya pesa za kukabiliana na changamoto za mazingira na
mabadiliko ya tabianchi katika eneo hilo
Mkuu
wa Idara ya Usafi na Mazingira Manispaa ya Ilala, Abdon Mapunda anasema
baada ya kukamilisha zoezi la ukusanyaji wa maoni ya wadau wa
mazingira, mfuko huo utaanza mara moja kabla ya mwaka 2015 kumalizika
Wakati
Manispaa ya Ilala ikiwa na jukumu la kusimamia uanzishwaji na
uendeshaji wa mfuko huo, ForumCC wao wanajukumu la kutoa msaada wa
kitaalamu ili kuhakikisha kuwa mfuko huo unafanikiwa na kufikia lengo
lililokusudiwa.
Mtaalamu
wa Misitu na Mazingira, Kahana Lukumbuzi ambaye alikuwa na jukumu la
kutengezeza andiko la uanzishwaji wa mfuko huo, akitoa ufafanuzi wa
baadhi ya vipengele vilivyomo kwenye andiko hilo.
Wadau wa mazingira wakifuatilia mkutano huo.
Sehemu ya mapendekezo ya namna Mfuko wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi utakavyokuwa.
Wadau wa mazingira wakifuatilia mkutano huo.
Wadau wa mazingira wakifuatilia mkutano huo.
Picha zote na Tabianchi.
No comments:
Post a Comment