Mnyika Aibukia Sakata la Bandari, Asema Dawa ya Jipu Sio Kulitumbua - LEKULE

Breaking

9 Dec 2015

Mnyika Aibukia Sakata la Bandari, Asema Dawa ya Jipu Sio Kulitumbua



Baada ya kuwa kimya tangu ashinde Ubunge, Mbunge wa Kibamba kwa tiketi ya Chadema, John Mnyika ameibukia kwenye sakata la ubadhirifu kwenye Mamlaka ya Bandari nchini na kuitaka serikali kuweka wazi ripoti za Dk. Harrison Mwakyembe na Samwel Sitta.
Mnyika ameyasema hayo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amedai kuwa ripoti za Sitta na Dk. Mwakyembe zimebeba ukweli zaidi kuhusu kinachoendelea bandarini hivyo kuziweka wazi kutasaidia kutibu tatizo lililopo zaidi ya kuwasimamisha watendaji waliotajwa.
Akiyafananisha matatizo ya bandari na majipu anayoyatumbua rais John Magufuli, alisema kuwa dawa yake ni kuyapasua ili kuondoa kiini badala ya kuyatumbua tu.
“Dawa ya jipu sio kulitumbua bali ni kulipasua ili kiini cha ndani kitoke, ukikiacha jipu linaazna upya tena linakuwa hatari zaidi,” alisema Mnyika.

“Kama kweli serikali ya awamu ya tano ina lengo la kufichua ufisadi, basi inapaswa kuweka wazi ripoti mbalimbali za uchunguzi ziwe dira ya kujua kiini cha matatizo kujitokeza katika Mamlaka ya Bandari,” aliongeza.

No comments: