Mhe. Jenista Aagiza Kamati Za Menejimenti Ya Maafa Nchini Kuwatoa Wanaoishi Kwenye Maeneo Hatarishi Mara Moja ......Vinginevyo Kamati Itawajibishwa


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UTEKELEZAJI WA AGIZO LA MENEJIMENTI YA MAAFA KWA KAMATI ZA MAAFA NGAZI ZA MIKOA, WILAYA, KATA NA VIJIJI

Kufuatia taarifa ya tahadhari ya uwezekano wa kuwepo kwa mvua za El-Nino iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Mwezi Agosti 2015, Ofisi ya Waziri Mkuu ilitoa agizo kwa Mikoa yote nchini kuchukua hatua za kujiandaa na kukabiliana na maafa yanayoweza kutokea kutokana na mvua hizo. 
 
Kamati za Maafa za Mikoa, Wilaya, Kata na Vijiji ambazo ndizo zenye jukumu kubwa la kusimamia masuala haya, hazijatekeleza agizo hilo kwa kuainisha hatua zilizochukuliwa katika Kuzuia/Kupunguza, Kujiandaa, Kukabili na Kurejesha hali baada ya maafa kutokea. Hivyo;
 
“Naagiza wenyeviti wa kamati za maafa katika ngazi husika kwa kushirikiana na taasisi na idara za serikali zinazohusika waorodheshe watu wote wanaoishi katika maeneo hatarishi na kuwapa barua za kuwataka kuhama mara moja katika maeneo hatarishi ili kuepuka athari za maafa. 
 
"Taarifa za utekelezaji wa agizo hili ziwasilishwe katika Ofisi ya Waziri Mkuu haraka sana kadri iwezekanavyo” amesema Mhe. Mhagama. 
 
Ili kutekeleza agizo hili ninaziagiza Kamati za maafa za Mikoa, Wilaya, Kata na Vijiji ziwajibike kutekeleza mambo yafuatayo;
 
I. Kamati zote ambazo hazijatekeleza maagizo yaliyotolewa na viongozi katika kushughulikia maafa zitoe maelezo ya kwanini hazijatekeleza maagizo hayo kwa mamlaka husika.
 
II.Endapo kutatokea maafa mahali popote katika nchi yetu kwa sasa, kamati za maafa zitawajibika kuelezea sababu za kutokea kwa maafa hayo ni nini katika maeneo yao na kuainisha hatua zilizochukuliwa na kamati hizo za kukabili hali hiyo iliyojitokeza. Lakini taarifa hizo pamoja na kuwasilishwa kwenye mamlaka husika pia ziwasilishwe kwenye vyombo vya habari. 
 
III.Kamati zote za maafa katika ngazi zote, zitoe maelezo na mipango waliyonayo juu ya kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu janga ambalo linasababisha maafa katika nchi yetu.
 
IV. Kamati zote za maafa katika ngazi zote, zishirikishe wadau wa maafa (Wananchi, Taasisi na Sekta binafsi) katika mipango yao yote ya kukabili maafa ya menejimenti ya maafa.
 
V.Kamati zote za maafa ziendelee kuratibu na kutoa taarifa juu ya misaada yote ya maafa inayotolewa na Serikali pamoja na wadau katika kusaidia waathirika wa maafa pale yanapotokea.
 
VI.Kamati hizo za maafa katika ngazi zote zinatakiwa, kuchukua /kumchukulia hatua mtendaji na mhusika mwingine yeyote ambaye hatatimiza wajibu wake na kutotekeleza maagizo yanayotolewa na viongozi nchini katika kukabili maafa mahali popote.
 
“Serikali inawaomba wadau wote wa maafa ushirikiano wa hali ya juu katika jambo hili muhimu katika nchi yetu ili kuweza kuokoa watanzania wengi ambao wanaweza kukumbwa na maafa kwa namna moja ana nyingine”, amesisitiza Mhagama 
 
Aidha, Sheria Na. 7 ya Mwaka 2015 ya Menejimenti ya Maafa inamtaka kila mdau kutekeleza wajibu wake katika suala zima la menejimenti ya maafa ikiwa pamoja na Kuzuia, Kujiandaa, Kukabili na Kurejesha hali baada ya maafa kutokea. 
 
“Napenda kuchukua fursa hii kuzikumbusha Kamati za maafa katika ngazi za Mikoa, Wilaya,Kata na Vijiji kuhakikisha kuwa zinatimiza wajibu wao katika suala zima la kushughulikia maafa kwa mujibu wa sheria” amesema Mhe. Mhagama. 
 
Hivi sasa sehemu mbalimbali za nchi yetu zimekuwa zikipata mvua nyingi ambazo zimesababisha maafa na baadhi ya sehemu zinakabiliwa na ukame. 
 
Taarifa nyingi zilizopokelewa zinaonesha baadhi ya maeneo ya nchi yetu yamekuwa yakipata mvua nyingi ambazo zimesababisha maafa bila Kamati za Maafa za Mikoa, Wilaya,Kata na Vijiji kuainisha hatua zilizochukuliwa katika Kuzuia/Kupunguza, Kujiandaa, Kukabili na Kurejesha hali baada ya maafa kutokea.
 
Iwapo juhudi za ngazi zote pamoja na Mkoa zitashindwa kukabili maafa yanayotokea katika ngazi za Wilaya, Kata na Vijiji, taarifa na maombi zitumwe katika ngazi ya Taifa kwa kuzingatia maelekezo/mwongozo wa uombaji wa misaada na utoaji wa taarifa za maafa uliotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Imetolewa na

JENISTA J. MHAGAMA (MB)
WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU
SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU

22 DESEMBA 2015
Previous
Next Post »
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Label

KITAIFA NEWS KIMATAIFA MICHEZO BURUDANI SIASA TECHNICAL ARTICLES f HAPA KAZI TU. LEKULE TV EDITORIALS ARTICLES DC DIGITAL ROBOTICS SEMICONDUCTORS MAKALA GENERATOR GALLERY AC EXPERIMENTS MANUFACTURING-ENGINEERING MAGAZETI REFERENCE IOT FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY ELECTRONICS ELECTRICAL ENGINEER MEASUREMENT VIDEO ZANZIBAR YETU TRANSDUCER & SENSOR MITINDO ARDUINO RENEWABLE ENERGY AUTOMOBILE SYNCHRONOUS GENERATOR ELECTRICAL DISTRIBUTION CABLES DIGITAL ELECTRONICS AUTOMOTIVE PROTECTION SOLAR TEARDOWN DIODE AND CIRCUITS BASIC ELECTRICAL ELECTRONICS MOTOR SWITCHES CIRCUIT BREAKERS MICROCONTROLLER CIRCUITS THEORY PANEL BUILDING ELECTRONICS DEVICES MIRACLES SWITCHGEAR ANALOG MOBILE DEVICES CAMERA TECHNOLOGY GENERATION WEARABLES BATTERIES COMMUNICATION FREE CIRCUITS INDUSTRIAL AUTOMATION SPECIAL MACHINES ELECTRICAL SAFETY ENERGY EFFIDIENCY-BUILDING DRONE NUCLEAR ENERGY CONTROL SYSTEM FILTER`S SMATRPHONE BIOGAS POWER TANZIA BELT CONVEYOR MATERIAL HANDLING RELAY ELECTRICAL INSTRUMENTS PLC`S TRANSFORMER AC CIRCUITS CIRCUIT SCHEMATIC SYMBOLS DDISCRETE SEMICONDUCTOR CIRCUITS WIND POWER C.B DEVICES DC CIRCUITS DIODES AND RECTIFIERS FUSE SPECIAL TRANSFORMER THERMAL POWER PLANT cartoon CELL CHEMISTRY EARTHING SYSTEM ELECTRIC LAMP ENERGY SOURCE FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 2 BIPOLAR JUNCTION TRANSISTOR 555 TIMER CIRCUITS AUTOCAD C PROGRAMMING HYDRO POWER LOGIC GATES OPERATIONAL AMPLIFIER`S SOLID-STATE DEVICE THEORRY DEFECE & MILITARY FLUORESCENT LAMP HOME AUTOMATION INDUSTRIAL ROBOTICS ANDROID COMPUTER ELECTRICAL DRIVES GROUNDING SYSTEM BLUETOOTH CALCULUS REFERENCE DC METERING CIRCUITS DC NETWORK ANALYSIS ELECTRICAL SAFETY TIPS ELECTRICIAN SCHOOL ELECTRON TUBES FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 1 INDUCTION MACHINES INSULATIONS ALGEBRA REFERENCE HMI[Human Interface Machines] INDUCTION MOTOR KARNAUGH MAPPING USEUL EQUIATIONS AND CONVERSION FACTOR ANALOG INTEGRATED CIRCUITS BASIC CONCEPTS AND TEST EQUIPMENTS DIGITAL COMMUNICATION DIGITAL-ANALOG CONVERSION ELECTRICAL SOFTWARE GAS TURBINE ILLUMINATION OHM`S LAW POWER ELECTRONICS THYRISTOR USB AUDIO BOOLEAN ALGEBRA DIGITAL INTEGRATED CIRCUITS FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 3 PHYSICS OF CONDUCTORS AND INSULATORS SPECIAL MOTOR STEAM POWER PLANTS TESTING TRANSMISION LINE C-BISCUIT CAPACITORS COMBINATION LOGIC FUNCTION COMPLEX NUMBERS ELECTRICAL LAWS HMI[HUMANI INTERFACE MACHINES INVERTER LADDER DIAGRAM MULTIVIBRATORS RC AND L/R TIME CONSTANTS SCADA SERIES AND PARALLEL CIRCUITS USING THE SPICE CIRCUIT SIMULATION PROGRAM AMPLIFIERS AND ACTIVE DEVICES BASIC CONCEPTS OF ELECTRICITY CONDUCTOR AND INSULATORS TABLES CONDUITS FITTING AND SUPPORTS CONTROL MOTION ELECTRICAL INSTRUMENTATION SIGNALS ELECTRICAL TOOLS INDUCTORS LiDAR MAGNETISM AND ELECTROMAGNETISM PLYPHASE AC CIRCUITS RECLOSER SAFE LIVING WITH GAS AND LPG SAFETY CLOTHING STEPPER MOTOR SYNCHRONOUS MOTOR AC METRING CIRCUITS APPS & SOFTWARE BASIC AC THEORY BECOME AN ELECTRICIAN BINARY ARITHMETIC BUSHING DIGITAL STORAGE MEMROY ELECTRICIAN JOBS HEAT ENGINES HOME THEATER INPECTIONS LIGHT SABER MOSFET NUMERATION SYSTEM POWER FACTORS REACTANCE AND IMPEDANCE INDUCTIVE RESONANCE SCIENTIFIC NOTATION AND METRIC PREFIXES SULFURIC ACID TROUBLESHOOTING TROUBLESHOOTING-THEORY & PRACTICE 12C BUS APPLE BATTERIES AND POWER SYSTEMS ELECTROMECHANICAL RELAYS ENERGY EFFICIENCY-LIGHT INDUSTRIAL SAFETY EQUIPMENTS MEGGER MXED-FREQUENCY AC SIGNALS PRINCIPLE OF DIGITAL COMPUTING QUESTIONS REACTANCE AND IMPEDANCE-CAPATIVE RECTIFIER AND CONVERTERS SEQUENTIAL CIRCUITS SERRIES-PARALLEL COMBINATION CIRCUITS SHIFT REGISTERS BUILDING SERVICES COMPRESSOR CRANES DC MOTOR DRIVES DIVIDER CIRCUIT AND KIRCHHOFF`S LAW ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS 1 ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS B ELECTRICAL TOOL KIT ELECTRICIAN JOB DESCRIPTION LAPTOP THERMOCOUPLE TRIGONOMENTRY REFERENCE UART WIRELESS BIOMASS CONTACTOR ELECTRIC ILLUMINATION ELECTRICAL SAFETY TRAINING FILTER DESIGN HARDWARE INDUSTRIAL DRIVES JUNCTION FIELD-EFFECT TRANSISTORS NASA NUCLEAR POWER SCIENCE VALVE WWE oscilloscope 3D TECHNOLOGIES COLOR CODES ELECTRIC TRACTION FEATURED FLEXIBLE ELECTRONICS FLUKE GEARMOTORS INTRODUCTION LASSER MATERIAL PID PUMP SEAL ELECTRICIAN CAREER ELECTRICITY SUPPLY AND DISTRIBUTION MUSIC NEUTRAL PERIODIC TABLES OF THE ELEMENTS POLYPHASE AC CIRCUITS PROJECTS REATORS SATELLITE STAR DELTA VIBRATION WATERPROOF