Magufuli Mgeni Rasmi Mkesha wa Kuiombea Amani Tanzania. - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Wednesday, 23 December 2015

Magufuli Mgeni Rasmi Mkesha wa Kuiombea Amani Tanzania.


RAIS John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkesha wa kuiombea Amani Tanzania utakaofanyika Desemba 31 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa ya Pentekoste (TFC), Godfrey Malassy alisema hayo jana jijini Dar es Salaam.
 
Alisema maandalizi yote yamekamilika ikiwemo kibali kutoka Polisi, pamoja na washiriki mbalimbali wa mkesha huo.

Askofu Malassy alisema mkesha huo utakuwa ni kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kuijalia nchi kumaliza Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu. Pia wanamwombea Rais Magufuli afya njema na utendaji mzuri anaoendelea kuufanya kwa maendeleo ya taifa.


Aidha Mwenyekiti huyo amewataka wananchi wote kutumia siku hiyo kumuomba na kumshukuru Mungu kwa amani iliyopo nchini kwa vile ndio msingi mkubwa wa shughuli za kila siku zinazosaidia kupata kipato na maendeleo ya nchi.
Post a Comment