Meneja wa operesheni wa
kampuni ya huduma za simu za mkononi ya Zantel, Gabriel Rafael ameuawa
kwa kupigwa risasi na majambazi.
Tukio hilo limetokea
jana saa 4:45 asubuhi eneo la ofisi za kampuni ya Nabaki Afrika, iliyopo
Mwenge, mita chache karibu na kampuni ya Coca-Cola.
Kamanda
wa polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alisema haikujulikana
mapema meneja huyo alikuwa akitokea wapi na gari lake aina ya Toyota
Double Cabin.
Alisema baada ya kupata taarifa za mtu
kuuawa kwa kupigwa risasi, polisi walifika eneo la tukio na kubaini kuwa
meneja huyo alikuwa amepigwa risasi kwenye kwapa la mkono wa kulia.
Kamanda Wambura alisema ndani ya gari la mfanyakazi huyo walikuta simu, laptop na fedha taslimu Sh1 milioni.
“Mwili
wake umepeleka kuhifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala na polisi
wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo pamoja na kuwasaka waliofanya
mauaji hayo,” alisema Wambura.
Taarifa za mauaji ya
meneja huyo zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii jana mchana
zikieleza kuwa, alikuwa akitokea benki kuchukua fedha.
Katika
hatua nyingine, Wambura alitoa rai kwa wakazi wote kutumia njia za
kiteknolojia kuchukua na kuhifadhi fedha badala ya kutembea nazo mfukoni
No comments:
Post a Comment