Dar es
salaam, Madereva wa boda boda wakiongoza maandamano ya kupinga ukatili
dhidi ya wanawake jijini Dar es salaam. Maandamano hayo yalianzia uwanja
wa Tipi ulioko Sinza hadi katika hotel ya Blue Pearl iliyopo Ubungo.
Dar es salaam, Ujumbe mbalimbali wa maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Kilimanjaro,
Maandamano yakipita eneo la kituo kuu cha Mabasi cha mjini Moshi
yakieekea katika viwanja vya kituo hicho ambako uzinduzi wa kampeni ya
siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini.
Kilimanjaro,
Mkuu wa wilaya ya Moshi, Novatus Makunga akisikiliza malezo kutoka
katika banda la shirika la NAFGEM linalopambana na vitendo vya Ukatili
dhidi ya Wanawake.
Mwanza,
Shirika la kutetea haki za wanawake la KIVULINI la jijini Mwanza
likikabidhi zawadi mbalimbali zikiwemo laptop kwa waandishi walioandika
habari zinazotetea haki za wanawake.
Kampeni
ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia inahitimishwa leo tarehe 10
Disemba ambayo ni siku ya kimataifa ya tamko la Haki za Binadamu ikiwa
ni ishara ya kuhusisha ukatili dhidi ya wanawake na haki za binadamu na
kutia msisitizo kwamba ukatili kama huu ni ukiukwaji wa haki za
binadamu.
Maadhimisho
haya yalianza rasmi tarehe 25 Novemba siku ambayo ilichaguliwa na Umoja
wa Mataifa mwaka 1993 kuwa ni siku ya kimataifa ya kupinga ukatili
dhidi ya wanawake ambapo kila mwaka, Umoja wa Mataifa unashauri,
mashirika ya Kimataifa na asasi zisizo za kiserikali kufanya shughuli
zinazolenga kufahamisha jamii juu ya ukatili wa kijinsia, hususani
ukatili dhidi ya wanawake.
Mwaka
huu, kauli mbiu inasema FUNGUKA, CHUKUA HATUA, MLINDE MTOTO APATE ELIMU
yenye lengo la kuhamasisha jamii kutambua changamoto mbalimbali
zinazohatarisha usalama na kuchochea ukatili wa kijinsia mashuleni ikiwa
ni pamoja na suala la viboko kuendelea kuwa tatizo kubwa, adhabu kali
wanazopewa watoto ambao haiendani na umri wao pamoja na mila na desturi
potofu zinazokandamiza watoto wa kike kama mimba za utotoni na
ukeketaji.
Mkurugenzi
wa shirika la WiLDAF, Dr. Judith Odunga akizungumza wakati wa ufunguzi
wa kampeni hizi alitaja changamoto nyingine kuwa ni miundombinu ambayo
ni pamoja na kuwa na madarasa ya kutosha, madawati, vyoo na sehemu za
kujisitiri kwa watoto wa kike, mabweni, uzio kuzunguka mashule pamoja na
mazingira magumu ya usafiri wakati wa kwenda na kurudi nyumbani na
kutokuwa na chombo cha wanafunzi cha kutumika kusemea matatizo yao pale
ambapo wanakutana na changamoto mbalimbali.
Akiongezea,
Dr. Odunga alisema kampeni hii kwa mwaka huu ilifanyika kikanda chini
ya uratibu wa mashirika na wadau mbalimbali wa maendeleo. Kanda hizo ni
kanda ya Ziwa (Mwanza, Mara na Shinyanga), Kanda ya Kaskazini (Manyara,
Arusha, Kilimanjaro na Tanga), Kanda ya Kati (Dodoma, Morogoro na
Singida), Kanda ya Kusini (Mtwara, Songea, Mbeya, Iringa na Lindi),
Kanda ya Pwani (Dar es salaam na Pwani) na kuratibiwa na wadau
mbalimbali wakiwemo mashirika ya KIVULINI, CWCA, NAFGEM, Morogoro
Paralegal, Mtwara paralegal, WiLDAF, TWCWC pamoja na Jeshi la Polisi.
Ujumbe wa maadhimisho haya na picha zinapatikana kupitia ukurasa wa Facebook wa WILDAF ambao ni www.facebook.com/WILDAFTZ
No comments:
Post a Comment