Inspekta Jenerali wa Polisi
(IGP), Ernest Mangu amelifumua Jeshi la Polisi nchini kwa kupanga na
kupangua vigogo wake, huku baadhi wakipandishwa nyadhifa.
Pangapangua
hiyo imewagusa pia maofisa waandamizi wa jeshi hilo walioko makao
makuu, makamanda wa mikoa, wakuu wa upelelezi wa mikoa (RCO) na wakuu wa
polisi wa wilaya (OCD).
Habari za uhakika kutoka ndani
ya makao makuu ya Jeshi la Polisi zinasema pangapangua hiyo imewagusa
pia wakuu wa vikosi, wakuu wa polisi wa vituo (OCS) na polisi wa vyeo
cha chini.
Akizungumza na Mwananchi jana, msemaji wa
polisi, Advera Bulimba alisema: “Mabadiliko hayo ni ya kawaida ya ndani,
hayana uhusiano na kasi ya Rais John Magufuli ila kazi lazima
ifanyike.”
Mabadiliko hayo yamekuja ikiwa ni siku
chache baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kukutana na maofisa wa
polisi kwenye Bwalo la Maofisa wa jeshi hilo Oysterbay jijini Dar es
Salaam na kati ya mambo yaliyotajwa ni kukumbushana utendaji,
uwajibikaji na mpango wa kulifumua jeshi hilo.
Chanzo
chetu ndani ya Jeshi la Polisi kimedokeza kuwa orodha ya waliokumbwa na
pangapangua hiyo ni ndefu na kwamba orodha ambayo Mwananchi iliiona ni
sehemu tu ya maofisa hao.
“Nafikiri IGP ameamua kusuka
upya safu ya uongozi ili kuboresha ufanisi katika utendaji wa kazi.
Unajua jeshi lazima liendane na falsafa ya Rais Magufuli (John) ya Hapa
Kazi Tu,” alidokeza afisa mwingine.
Mabadiliko hayo
yamekuja wakati tayari makamanda wa polisi wa baadhi ya mikoa wakiwa
wamebadilishwa katika vitengo walivyokuwa awali, wakiwamo Kikosi cha
Usalama Barabarani, ili kuboresha utendaji wa jeshi hilo.
Mabadiliko
Katika
mabadiliko hayo, Naibu Kamishina wa Polisi (DCP), Salehe Ambika
amehamishwa kutoka kitengo cha Sheria na Huduma za Utafiti kwenda kuwa
mkuu wa utawala.
DCP Robert Boaz amehamishwa kutoka
kitengo cha intelijensia kwenda kuwa mkuu wa kitengo cha uhalifu wa
kitaifa na uhalifu wa kupangwa au Transnational and Organized Crime
(TOC).
Katika panguapangua hiyo, Kamishna Mwandamizi wa
Polisi (SACP), Luteta Modest amehamishwa kutoka kitengo cha sheria
kwenda kuwa mkuu wa kitengo cha sheria na huduma za utafiti.
Mkoa wa Kilimanjaro umetikiswa zaidi na mabadiliko hayo
baada ya maofisa watano waandamizi kuhamishiwa vituo vipya na nafasi zao
kuchukuliwa na sura mpya.
Kamanda wa polisi wa mkoa
huo, Fulgence Ngonyani amehamishiwa Chuo cha Polisi Kilwa Road, na RCO
Ramadhan Ng’anzi amehamishiwa mkoa wa Shinyanga kuendelea na wadhifa
huo.
OCD wa Moshi, Mrakibu Mwandamizi Deusdedit Kasindo
amepanda cheo na kwenda kuwa kamanda wa Mtwara, wakati mkuu wa kitengo
cha FFU wa mkoa huo, amehamishiwa mkoa mwingine.
Katika
mabadiliko hayo, kamanda wa mkoa wa Iringa, Kamishina Msaidizi Ramadhan
Mungi amehamishiwa Kilimanjaro kuchukua nafasi ya Ngonyani anayekwenda
chuoni.
Nafasi ya RCO wa Kilimanjaro imechukuliwa na SSP Black Magesa aliyekuwa OCD Korogwe.
Kamanda
wa Mkoa wa Manyara, ACP Christopher Fuime amehamishiwa Kinondoni
kuendelea na wadhifa huo, wakati kamanda wa Ruvuma, ACP Mihayo Miskhela
amehamishiwa mkoani Tanga.
Pia, kamanda wa Mkoa wa
Tanga, ACP Zuneri Mumbeki amehamishiwa Ruvuma kuendelea na wadhifa huo,
huku kamanda wa Kinondoni, SP Camilius Wambura amehamishiwa Mkoa wa
Manyara kushika wadhifa huo.
Maofisa wengine ni Gerald
Ngichi, ambaye alikuwa OCD Magomeni, amehamishiwa Lindi, Nsekela M.
Nsekela (OCD Nyang’wale sasa ofisa mnadhimu II Rorya, Nesto Msembele
(OCD Mbalizi sasa Polisi Jamii Mbeya), William Malei (ofisa mnadhimu ll
Kigoma, sasa OCD Korogwe), Melard Sindano (OCD Kigoma, sasa OCD
Nyang’wale).
Wengine ni Patrilinius Mlowe (OC-CID
Kwimba, sasa OCD Kawe, Edson Kasekwa (OCD Makambako, sasa OCD Kilolo),
Agustino Titus (mnadhimu ll Morogoro, sasa OCS Malinyi).
Katika
pangua pangua hiyo, Raphael Msela (ofisi ya RCO Kagera, sasa naibu RCO
Kagera), John Samwel (OCS Malinyi, sasa ofisa mnadhimu II Morogoro), SP
Debora Mrema (polisi jamii Mbeya, sasa OCD Mbalizi, SP Omari Mtungu (OCD
Tanga, sasa OCD Moshi),SP Alfred Mwaikusa ambaye alikuwa OCS Singida
sasa anakwenda kuwa OC-CID Serengeti.
Wengine ni SP
Limited Mhongole ambaye alikuwa OC-CID Mbarali sasa anakuwa OCD Mbarali,
ACP Jaffar Mohamed (RPC Pwani, sasa makao makuu) na ACP Peter Kakamba
anakuwa RPC Iringa.
Pia ACP Mussa Taibu aliyekuwa RCO
Shinyanga, sasa anapelekwa upelelezi makao makuu, SSP Pili Omari (OCD
Kawe, sasa OCD Mwanga, David Chidingi (OCD Lindi, sasa OCD Magomeni, SSP
Constantiono Mbugambi (OCD Mwanga, sasa OCD Ngara), SSP Jullius Lukindo
(OCD Mbarali, sasa OCD Mvomero).
No comments:
Post a Comment