Kumekuwa na nchi nyingi zikijitahidi kupambana na ishu ya dawa za kulevya Duniani, nchi nyingine imefikia mpaka hatua ya kuweka sheria kali ili kudhibiti kabisa kuingizwa na matumizi ya dawa hizo.
Kwenye list ya nchi ambazo zinatajwa watu wake wengi kukamatwa kwa dawa za kulevya, Nigeria nayo imo !! stori za Wanigeria wengi kutajwa na kukamatwa na dawa za kulevya zimesikika na kugusa pia vichwa vya habari.
Kilichonifikia kutoka Malaysia ni ishu ya Mnigeria mmoja, Ekene Collins Isaac ambaye amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya miaka mitatu iliyopita nchini humo.
Ekene Collins Isaac alikamatwa akiwa amemeza kusafirisha dawa hizo aina ya methamphetamine zenye uzito unaokaribia kilogram moja.
No comments:
Post a Comment